Timu ya Taifa, kilimanjaro Stars Leo imecheza mechi yake ya kwanza ya CECAFA Challenge Cup na timu ya Taifa ya Zambia katika mji wa Machakos, ambao uko takriban kilometa 60 kutoka Nairobi. Timu hizo zimefungana 1-1. Kwa ujumla mchezo ulikuwa mkali na wa kusisimua sana, Katika mechi iliyotangulia ambayo iliwakutanisha Burundi NA Somalia, Burundi iliwafunga Somalia goli 2. Yafuatayo ni matukio katika picha
Hapa vijana wetu wakiwa katika Picha ya Pamoja Kabla ya kwanza kwa kipindi cha kwanza
Bwana shiyo Pamoja na Gavana wa Machakos wakiwasalimia wachezaji.
Hongera stars ...fanyeni kweli kwa mechi zijazo bado safari ni ndefu kuna timu za kutisha kama ethiopia na uganda...
ReplyDeleteHuyu Gavana Mutua ana maono makubwa kwa ajili ya Kaunti yake ya Machakos. Anatoa ardhi kwa wawekezaji ili wajenge mji mpya. Najua ipo mikoa iliyokwisha alika wawekezaji na yenye master plan zinazoeleweka lakini siyo yote. Hii ni challenge kwa wakuu wa mikoa je mna maono gani ya kutaka mikoa na wilaya ziwe na miji na vijiji vya kisasa?.
ReplyDelete