WAAFRIKA wametakiwa kukataa utumwa na kuiga neno la ‘WOOD’, kwenye soko la filamu hasa baada ya nchi nyingi kukopi jina la ‘HOLLYWOOD’ ambalo ni eneo lililopata umaarufu mkubwa kwenye soko la filamu Duniani kwa kuwa na wasanii nyota na studio za kisasa, za masuala ya filamu.
Akielezea mapema leo kwenye semina ya waandishi wa habari za Sanaa kuhusu Filamu za Afrika, Mkurugenzi wa Tamasha la Filamu za Kiafrika la Arusha (Arusha African Film Festival –AAFF 2013) na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Arcadia, kilichopo Pensylvania, Marekani , Mr. Akpor Otebele, alisema Waafrika waache dhana ya kuendelea kutumia jina hilo ambalo nchi nyingi wamekuwa wakitumia viunganishi vya neon hilo la ‘Wood’ bila kujua maana hasa la kuendelea kulitumia.
Hii haina maana, ni la kuliacha na Nigeria kule waigizaji wengi wanatafakari maana ya hili neno lakini jibu hakuna, lakini bado wanaendelea kulitumia” alisema.
Akitolea mfano wa baadhi ya nchi zinazotumia jina hilo kutoka Hollywood, ni pamoja na : Bongowood/ Swahiliwood (Tanzania), Nollywood (Nigeria), Riverwood (Kenya), Ghollywood (Ghana), SierraWood (Sierra Leone)na Congowood (Kongo) na mengine mengi.
Akpor Otebele aliongeza kuwa, kuendelea kutumia viunganishi hivyo ni kuwanufaisha watu wa Magharibi na kuupamba Mji wa Hollywood unaoishi mastaa na studio maalufu huko Lose Angels nchini Marekani, ambapo kwa dhana hii inafanya Waafrika kuwa watu wasiojua wanachokifanya.
…”Swahiliwood, its means, Swahili ubao? Is that sure? So why to use ‘Wood’?? in Swahili meaning ‘UBAO’?? Alisema Akpor Otebele.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Arcadia, kilichopo Pensylvania, Marekani Bw. Akpor Otebele, akiongea kwenye semina hiyo jijini Arusha leo 
Juu na chini ni washiriki wa semina ya waandishi wa habari za Sanaa kuhusu Filamu za Afrika, iliyoandaliwa na Tamasha la Filamu za Kiafrika la Arusha (Arusha African Film Festival –AAFF 2013)
NI Kweli, Manake Mi navyojua Bongo movie NI maarufu kuliko Hy Bongowood Ila wachezaji wenyewe ulimbukeni Ndo Maana wanalazimisha bongowood
ReplyDeleteWaambie hao. Wanaiga hadi majina ya wasanii.
ReplyDeletewaambie hao!!
ReplyDeleteSawa, wabongo wengi ni wavivu wakufikiri, nimeona hata ktk sinema zetu baki ya maudhui kuwa ya ki nigeria lakini hata muziq wakusindikiza sinema unakuwa wa kinigeria, aibuuu, ni kukosa elimu na kujitambua, jamani copy n paste hata tamthilia?
ReplyDeleteBONGOWOOD well, naona neno limewatia jamaa upupu.Lugha is a kinetic thing, its like a living organism, if it does not grow, if its not allowed to breathe freely it will die. This is neologism and more recently there have been numerous memes. Did you know bwana profesa kuwa SELFIE sasa ni neno kwenye kamusi? Tumekopa maneno mengi katoka lugha mbalimbali, tumeunda maneno mengi pia,jambo kubwa ni tusichafue hali ya hewa tu kama asemavyo mjomba..
ReplyDeleteHuyo mdau hapo juu anayezungumza kuwa wabongo wengi ni wavivu wa kufikiri......Is he serious...yeye hapa afanyaje? Ni kama nyani kumcheka tumbiri.
ReplyDelete