Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akikagua mradi wa mgodi
wa makaa ya mawe wa kampuni ya Tancoal katika eneo la Mtunduwalo, Mbinga
mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013. Kinana alitembelea mgodi huo, kufuatia
mgogoro uliopo kati ya wananchi na uongozi wa mgodi kuhusu masuala
mbalimbali ikiwemo malipo ya fidia kwa maeneo yalitochukuliwa.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya
kukabidhi pikipiki 50 zilizotolewa na mbunge kwenda kwa watendaji wa
vijijini.
Kijana
Bonus Hyera wa kijiji cha Lusewa, akimsalimia kwa kumbusu mikono kwa
shauku, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose
Migiro, baada ya Dk. Asha-Rose kukutana na kijana huyo, wakati wa
shughuli ya uzinduzi wa tawi la CCM Kata ya Mbinga mjini, mkoani Ruvuma,
Nov 20, 2013, uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Kijana huyo aliyeonekana kama aliyekuwa amelewa kiasi, alionyesha
heshima kubwa kwa Dk. Asha-Rose, tofauti ilivyokuwa inadhaniwa na baadhi
ya watu waliopomuona akimsogelea kwa shauku kiongozi huyo.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kijiji cha
Aman Makolo waliojitokeza nyumbani kwa Balozi Hilda Komba wa shina namba
9 ,Tawi la Amani Makolo wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma.
Wanachama
wapya wa Tawi la Amani Makolo wilayani Mbinga wakila Kiapo cha
Uanachama wa CCM mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
ambaye leo amefanya ziara katika wilaya ya Mbinga.
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma ya Mganda wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano wilayani Mbinga.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimueleza Katibu wa NEC Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose uzoefu wake wa kuendesha
pikipiki,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Ndugu Senyi Ngaga.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Mbinga
mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanika kwenye viwanja vya michezo
vya Mbinga mjini ambapo aliwaeleza wananchi kuwa chama cha Mapinduzi
kitasaidia kutoa ushauri kwa mazao ambayo bei yake inashuka na kupanda.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa Wilaya wa zamani Ndugu Osmund Kapinga.
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana
na Mzee Osmund Kapinga Mkuu wa Wilaya mstaafu mara baada ya kukamilika
mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya michezo vya Mbinga mjini mkoa wa
Ruvuma.
Hapo panapolimwa panafaa kulimwa kwa trekta.
ReplyDeleteKinana na timu yako mnafanya very good job kwa sasa ila ningeomba itoke rohoni isiwe tu kuelekea 2015 na ushauri wa bure hata mngejigalagaza kwenye matope nadhani you have a long way to go kuwaridhisha watanzania na moja muhimu amabalo sikufichini ni jitihada za wazi za kuridhisha za kupambana na Rushwa otherwise yote yatakuwa diluted
ReplyDelete