LOWASA PHOTO
Damas Makangale, Mhariri MOblog.

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa mara nyingine tena ameibuka na kauli ambao alishawahi kuitoa huko nyuma ya viongozi wa Serikali ya awamu ya nne kushidwa kuchukua uamuzi mgumu kwa maslahi mapana ya taifa.

Lowassa alitoa kauli hiyo mjini Dodoma katika kikao cha bunge kinachoendelea akisema nchi inakosa viongozi jasiri wenye kusimamia utekelezaji wa mambo waliyoamua katika Nyanja mbalimbali za maendeleo.

“wananchi, wanasiasa, wabunge, viongozi wanalalamika hatuwezi kuwa na jamii ya kulalamika lazima mtu mmoja ajitokeze na kufanya maamuzi magumu lazima ajivishe joho la ujasiri ili mambo yaende,’ amesema Lowassa.

Amesema nchi ina tatizo kubwa la uswahili mwingi wa kukaa na kushidwa kutekeleza mambo yaliyoamualiwa kwenye vikao kiasi cha kufanya kila mtu kulalamika kwa wakati wake.

Lowassa amesema kuwa hata matokeo makubwa sasa au “Big results Now” haiwezi kutekelezwa kwa sababu ya uswahili na mazingira ya hapa Tanzania na Malaysia ni tofauti hapa ni uswahili tu ndio unaosumbua taifa letu lishindwe kusonga mbele.

“Tukishakubaliana mambo ni lazima yafanyike. Ni lazima tuondokane kuwa nchi ya kulalamika kuanzia kiongozi wa juu mpaka mwananchi,” alisisitiza.

Sisi kama MOblog tunaungana na Lowassa katika kutekeleza mipango ya serikali kama ilivyopangwa bila woga wala kigugumuzi lazima viongozi wote waliopewa dhamana ya kuongoza waongoze kwa vitendo waache uswahili ili taifa liweze kusonga mbele.
Kusoma zaidi ingia hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kwa kweli kwa hili mh Lowassa amenena na wengi tunaiunga mkono kauli yake kwani nchi imejaa uswahili.Haiingii akilini kiongozi kusimama na kupindisha sheria.Mpaka nchi itakapoamua kuheshimu sheria ndipo tutaendelea.nchi zilizoendelea sheria ni sheria hata awe nani havunji as far as iko wazi na hakuna uonevu na kila mtu akishajua hivyo haileti shida ila uswahili, siasa uswahiba na uafrika mi naona ni kansa ya maendeleo

    Mdau UK
    Sina chama

    ReplyDelete
  2. Kwani mswahili ni nani? au uswahili ni nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...