Si jambo geni tena hivi sasa nchini Tanzania kusikia fulani kashambuliwa au kauawa kwa risasi.
Silaha za moto hapa nchini hasa zile zinazomilikiwa kiholela zimekuwa zikimilikiwa na kila anayetaka... kama vocha za simu. Hata mtu mwenye uwezo kidogo, na asiye na sababu ya kuwa na silaha anaweza kumiliki silaha nyumbani kwake. Bastola kwa sasa zimekuwa kama bidhaa ya utashi na watu wanazimiliki kama wanavyomiliki simu za mkononi.
Ungana na Sophia Kessy (L) na Mubelwa Bandio (R) katika sehemu hii ya kwanza kuangalia tatizo hili linaloonekana kuzidi kuathiri na kutishia maisha ya waTanzania wengi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Maajabu na Miujiza ya umilki wa Bastola Tanzania:

    Imekuwa ni Fasheni kwasasa unakuta mtu hata Mtaji wa LAKI TATU KWAKE MGOGORO, HUKU AKIWA NA UPUKU PUKU WA MADENI NA SHUGHULI ZAKE HAZIELEWEKI lakini Bastola kiunoni!!!

    ReplyDelete
  2. Hizi zama za Dijitali Watanzania wengi wetu zinatu changanya.

    Tunadhani maana yake ni Umiliki wa Silaha na hasa Bastola!

    ReplyDelete
  3. Utafiti ukifanyika inawezekana kabisa zaidi ya 75% wanaomiliki Bastola hawastahili kwa vigezo kuzimiliki!

    Tunaweza kushangaa kukuta Mmiliki wa Genge ama Chinga mwenye mauzo mazuri anapata sifa za kumiliki Bastola kwa kigezo cha Mapesa anayozungusha mkononi kuliko Mabosi wetu wa Kipedeshee ambao wengi wanaishi kwa Mabao, Vimeo na Madeni makubwa (KIMUONEKANO KWA NJE WAKIWA MABOSI NA KIHALISIA WAKIWA MAFUKARA)!

    ReplyDelete
  4. Naona tatizo sio umiliki. Tatizo ni anaye miliki amefanyiwa 'psychological evaluation'?
    kuna wengine wana matatizo ya akili(medically) lakini hajijui wala anayemlikisha silaha hajui namna ya ku-evaluate. Umiliki wa busara ni muhimu (azma za leo usalama ni hafifu; inabidi mtu ujilinde wewe na familia yako)
    RIP Dr. Mvungi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...