Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika Kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kiongozi mwandamizi wa chama cha NCCR Mageuzi, marehemu Dkt. Sengondo Mvungi, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Kibamba Msakuzi, jijini Dar es Salaam, leo mchana kwa ajili ya kuifariji familia ya marehemu na kutoa mkono wa pole. Mwili wa marehemu unatarajia kuwasili nchini kesho ukitokea nchini Afrika ya Kusini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Kibamba Msakuzi, jijini Dar es Salaam, leo mchana kwa ajili ya kuifariji familia ya marehemu na kutoa mkono wa pole. Mwili wa marehemu unatarajia kuwasili nchini kesho ukitokea nchini Afrika ya Kusini. Picha na OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...