Na Woinde Shizza,Arusha

BENDI inayotamba kwa sasa hapa na ambayo imechukuwa tuzo mbalimbali za muziki hapa nchini (MASHUJAA BAND) jumamosi November 16 inatarajia kushuka jijini Arusha katika ukumbi wa triple A kuwapa burudani wakazi wa jiji hilo na vitongoji vyake.

Akiongea na waandishi wa habari jijini hapa,muandaaji wa onyesho hilo kutoka katika kampuni ya Rickenet Intertament Papa Ernest alisema kuwa bendi hii ya mashujaa itatua jijini hapa kwa ajili ya onyesho hilo ambapo alilifafanua kuwa tangu kuanzishwa kwa bendi hyo,hili litakuwa ni onyesho lao la kwanza kufanya jijini hapa.

Alisema kuwa bendi nzima ya mashujaa inatarajiwa kutia timu jijini hapa likiwa na wanamuziki wake wote ambapo alimtaja kiongozi wa bendi hiyo kuwa ni na Chaz Baba,

Alitaja kiingilio cha onyesho hilo kuwa ni shilingi 10000 kwa kila mmoja huku akiwasihi wakazi wa mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi kuangalia bendi hii ambayo inawanamuziki wengi ambao wanajua kutawala jukwaa kwa uhodari wao wa kuimba pamoja na kucheza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...