Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akifungua rasmi warsha ya siku moja ya viongozi wa kimila wa jamii ya wafugaji kuhusu afya ya uzazi na kuzuia maambukizi ya ukimwi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere hapa Dar tarehe 9.11.2013.
Mke wa RaiS Mama Salma Kikwete akivishwa mavazi ya wafugaji wa jamii ya wamasai wakati wa warsha ya viongozi wa kimila iliyofanyika Dar tarehe 9.11.2013. Baadaye Mama Salma alipokea zawadi kwa ajili ya Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Nadhani hii ni hatua nzuri sana ya kuwaleta karibu jamii ya wafugaji ili kupitia viongozi wao wa kimila elimu hii ya afya ya uzazi na jitihada za kuondoa/kupunguza maambukizi ya vvu iweze kuwafikia walengwa wa kundi hilo .... nadhani hata baadhi ya mila potofu zinaweza kutokomezwa kupitia kampeni za elimu zikianzia kwa viongozi wa kimila na kuwapa wao jukumu la kusimamia jamii zao.....Hongera kiongozi wa WAMA & hongera 1st Laddy Mama Salma JK

    ReplyDelete
  2. Mama umependeza sana.Basi tuliweke kuwa vazi la kitaifa uwe unalipeperusha nje ya nchi mama.umependeza sana

    ReplyDelete
  3. Mama hebu angalia kwa jinsi ulivyopendeza kwenye hayo MAVAZI YA KIMASAI? Sasa kama nyie wakuu wa nchi muamue kusema kuanzia leo wanawake wote WAKITANZANIA WAVAE MAVAZI KAMA HAYO NA KICHWANI WANYOE VIPARA,,hakiyamungu mm ni MLUGURU wa kule mji kasoro bahari,lakini mm ningukua wa kwanza kuwavalia njuga watu wangu wote wa moro kuyavaa hayo mavazi ya KIMASAI maana tushachoka na mavazi ya ajabu ajabu kama vile MITAITI na MIWIGI,na vyote hivyo vipigwe malufuku,,na kwa upande wa WANAUME ya shonwe mavazi maalum yenye NAKSHI YA RANGI YA BENDERA YA TAIFA LETU,,walahi tungependeza wote kwa pamoja kama NDEGE TAUSI au KASUKU,, naitwa mdudu kaka kuona nipo huku UINGEREZA,,,na kama tutavaa hayo mavazi basi tujiandae na mapokezi makubwa ya WATALII KUTOKA KONA ZOTE ZA HII DUNIA,,haya ni hayo tu kwaleo,,mkaee kwa amani na upendo huko nyumbani nawapendeni wote,,ila nawaomba mlifanyie kazi hilo swala WADAU WOTE WA MICHUZI BLOG,

    ReplyDelete
  4. SSAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAFI SSSSSSSSSSSAAAAAAAAAAAANNNAAAAA!

    Hutuna haja ya kwenda nje ya Tanzania kutafuta vazi la taifa. Twendeni vijijini!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...