MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa (CCM) Lita Kabati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake mwishoni mwa wiki.(picha na Denis Mlowe).
========  ======  =======
MBUNGE AVITAKA VYOMBO  VYA DOLA KUTENDA HAKI
Na Denis Mlowe,Iringa
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa (CCM) Lita Kabati amevitaka vyombo vya sheria hususan mahakama na Jeshi la Polisi kutenda haki kwa watuhumiwa wanaofika katika idara hizo wanapopatwa na matatizo na kesi mbalimbali.

Akizungumza na mwandishi wa habari Ofisini kwake Kabati alisema hayo baada ya kutembelea Idara ya Magereza ya Mkoa wa Iringa na kukutana na wafungwa na mahabusu walimpatia kero zao kwa lengo la kuzifikisha katika mamlaka husika.

Alisema watuhumiwa wengi wamevitupia lawama vyombo hivyo kwa kuwasingizia kesi mbalimbali hususani jeshi la polisi na kwa upande wa mahakama kutoa vifungo ambavyo wengi wao wamembakiwa na jeshi hilo.

kabati alisema mahakama na jeshi la polisi vinatakiwa kufanya uchunguzi wa kina katika kubaini makosa ya watuhumiwa na kutenda haki kwa kufata sheria za nchi kuliko ilivyo sasa wengi walioko katika kifungo na mahabusu wanalalamika kutondewa haki na kubambikiwa kesi ambazo haziwahusu.

 "Mahakama ni moja ya vyombo vya vinavyotetea haki ya mtuhumiwa hivyo kama mtu ametenda uhalifu kwa namna yoyote lazima uchunguzi wa kina ufanyike kwa lengo la kutenda haki kwa watuhumiwa, wengi wao wametoa malalamiko kuhusu jeshi la polisi na mahakama kuwa rushwa inatawala katika vifungo vyao na wanaomba msaada wa kusaidiwa kutendewa haki" alisema Kabati

Alisema viongozi wako kwa ajili ya kutetea haki za msingi za mwananchi na rasilimali zake na kumletea maendeleo hivyo mahakama na jeshi la polisi waepuke kuwabambikia kesi wananchi.Kabati alisema lazima tuwe wakweli  jeshi la polisi limekuwa likielemewa kwa kiwango kikubwa tuhuma za kuwanyanyasa na kuwakandamiza watuhumiwa kutokana  na malalamiko kutoka kwa wafungwa na mahabusu wenyewe kwa hili linatakiwa kubadilika.

"Imenisikitisha sana kwa kuwa kuna watu wanajifanya Miungu mtu katika hizi Idara za mahakama, na jeshi la polisi kuweza kuwabambikia kesi watu hivyo kusababisha mrundikano mkubwa wa kesi mahakamani na kujaza watu katika magereza zetu, mie naomba kabisa wazifatilie na hili jambo sitalifumbua macho kuanzia sasa na nitalivalia njuga na nitahakikisha kwamba katika ubunge wangu nilionao hizi changamoto zinatatuliwa kwa wakati" alisema Kabati.

alisema atapigia haki ya wananchi wa Iringa kutoendelea kunyanyasika na vyombo hivi vya dola  kwa kupakaziwa kesi ambazo haziwahusu na kila mwananchi ana haki ya kutendewa yaliyo mazuri kwa kufuata sheria za nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...