MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili Solomon Mukubwa atashiriki Tamasha la Krismasi lililopangwa kufanyika Desemba 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa tayari wamemalizana na Mukubwa, ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya.

“Pia tumemalizana na mwimbaji wa hapa nchini anaitwa John Lissu ambaye ni mmoja kati ya waimbaji mahiri na wenye mashabiki wengi.

“Dhamira yetu ni kuwa na wasanii wote wanaokubalika na mashabiki,” alisema Msama na kuongeza kuwa Desemba 26 mwaka huu tamasha hilo litafanyika Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Mukubwa ametamba na albamu mbalimbali ikiwemo Usikate Tamaa, ambayo ina nyimbo kama Mungu Wangu Nitetee, Niko na Yesu, Mke Si Nguo, Moyo Tukuza Bwana, Chunga Ahadi Yako na Yesu Jina Zuri na Usikatae Tamaa. Pia Mukubwa amewahi kutoa albamu mbili ambazo ni Sijaona Rafiki na Mungu Mwenye Nguvu.

Sijaona Rafiki Kama Yesu ambayo ni albamu yake ya kwanza ina nyimbo za Uwe Nami Bwana, Sijaona Rafiki Kama Yesu, Nitayainua Macho, Matendo ya Mungu, Bwana Wastahili na Yesu Kimbilio. 

Wasanii wengine ambao tayari wamethibitisha kushiriki tamasha hilo la nyimbo za kusifu na kuabudu ni Watanzania, Rose Muhando, Upendo Nkone na Upendo Kilahiro wakati wa nje ni Ephraim Sekeleti wa Zambia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...