Baadhi ya Wafanyabiasha wakiwa mahakamani kujua hatma ya Mfanya
Biashara Haji Mohamed Mpemba alieitwa mahakamani kujibu shitaka la
kutolipa kodi ya Huduma ambayo wafanyabiasha wanaikataa kwa kutozwa
nje ya Taratibu zilizopo
 Maduka ya Manispaa ya Lindi yakiwa yamefungwa leo ikiwa siku
ya pili mfulizo ambapo wafanyabiashara wakiwa wamekutana katika Ukumbi  M M hotel kuunda Umoja wao ili kupinga ongezeko la kodi mbalimbali pamoja na Mpango wa Mashine za TRA kwa Wafanyabiashara wadogo.

 =======  =======  =======
Na Abdulaziz Video
Wakazi wa Manispaa ya Lindi Wameendelea kukosa huduma ya kununua
bidhaa za madukani ikiwemo vyakula  kwa siku ya pili mfululizo
kufuatia mgomo ulioitishwa na wafanyabiashara kutokana na kodi kubwa
inayotozwa na mamlaka ya mapato ikiwemo kodi ya huduma inayotozwa na
halmashauri ya manispaa ya Lindi

Kufuatia mgomo huo wafanyabiashara hao walikutana katika ukumbi wa
Double M hotel na kuazimia kuendelea na mgomo hadi wenzao
waliofikishwa mahakamani kwa ajili ya kodi ya Huduma kuachiliwa

Habari zaidi tutawaletea hapo baadae..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Msishindane nao,wapeni siku tatu tu, watarudi wenyewe. Kwanini kila mtu anataka kubembelezwa siku hizi? Kumbukeni hii nchi ni yetu sote Watanzania na hakuna mwenye haki kumzidi mwenzake.

    ReplyDelete
  2. Chondechonde serikali mkifanya mchezo kwenye kukusanya mapato tutajuta,,ikumbukwe ya kwamba muungano wa EAST AFRICA unaenda kufa kwa upande wetu so msifanye mchezo kwenye eneo hilo,hao wanaogoma vitu vyote vichukuliwe viwe chini ya serikali ndio itakua mwalubaini wao na kwa wengine pia,jamani ndugu zangu watanzania mm huku nilipo UINGEREZA kama utaenda kinyume na matakwa ya serikali basi maisha yako yatakua na uzito wa sufi,, ndio maana wenzetu wameendelea na kupiga hatua kubwa sn mbele coz hawana masihara kabisa na hayo mambo ya UKUSANYAJI WA MAPATO,,amkeni kwenye usingizi na muwe wepesi wa kulipa hizo kodi kwa faida ya NCHI YAKO,naitwa mdudu kakakuona,

    ReplyDelete
  3. Manispaa ikipata kodi ikumbuke kuweka lami sehemu hizo pia

    ReplyDelete
  4. Sisi wafanyakazi wa Serikali huwa tunakatwa kodi kubwa sana (asilimia thelathini ya mshahara wako) lakini wafanyabiashara wao wamepewa mashine hawataki kuitumia wanaogopa kodi.

    Kama alivyosema mdau hapo juu mukifanya dharau basi tutaangukia pua?

    TRA jee munajua kwamba baadhi ya wafanya biashara wakubwa hapo uhindini huwa wanaficha hizo EFD zenu na ukienda kununua bidhaa wanakwambia eti njoo kesho maana leo mashine imeharibika?

    FUATILIENI MUTAWAONA.

    ReplyDelete
  5. wee unaye ongea wa pili, huna wala hujui biashara, makampuni ya kuchimba madini yanapakua na hawalipi chochote, mzawa na kabiashara chake unataka ukamue, embu nenda ukafikirie mara mbili juu ya ulichokiandika, wafanyabiashara hajakataa kulipa kodi,wanapinga uongezekaji wa kodi, na installation ya machine za TRA

    ReplyDelete
  6. mdau wa maoni wa pili ni sawa unayosema .LAKINI juwa kuwa hapa UIENGEREZA (UK) the system is fair and transparent sio kama huko BONGO.
    Kwani nani hajuwi kuwa kuna matajiri wakubwa tu hawalipi kodi ? Munawabana hao masikini tu. Kama anavyosema rafiki yangu 'its always poor who suffer.
    Pia wafanya biashara kule zanzibar munawalipisha kodi mara mbili yaani ZRB na TRA ndani ya nchi moja ya TANZANIA !.
    Hivi sasa hapa UK Wales watakuwa na tax system yao bila ya kuingiliwa na westminster nategemea kuwa umesikia camera man akisema hivi karibuni.

    ReplyDelete
  7. Kusanyeni kodi na weka siasa pembeni na hakikisheni kodi yetu inatumika vizuri na si vinginevyo. Jamani kodi ndio kila katika maendeleo; mdau anasema makampuni makubwa yanakwepa kodi nae ametulia kimya na anataka wengine nao wakwepe sasa maendeleo yatakuja kwa miujiza ipi!

    ReplyDelete
  8. Nimependa HAKIMU'S OFFICE!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...