Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiburudika kwa kucheza muziki sambamba na wakina Mama wakazi wa Kata ya Saranga,Kimara jijini Dar es Salaam,Mwishoni mwa wiki wakati alipokwenda kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya pili ya Sekondari katika Kata hiyo.Zaidi ya Sh. Mil. 100 ziliweza kupatikana kwenye harambee hiyo.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipena mikono na Wakazi mbali mbali wa Kata ya Saranga,Kimara wakati akiendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya pili ya Sekondari katika Kata hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisisitija jambo kwa wananchi wakazi wa Kata ya Saranga,Kimara jijini Dar es Salaam wakati wa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya pili ya Sekondari katika Kata hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hata kama ni kwa malengo ya kisiasa lakini unategemea mwanasiasa atafanya jambo katika siasa lisiwe kabisa na malengo ya kisiasa?

    N'nachoona hapa lazima tukubali kuwa lililo la muhimu ni ukweli kuwa hatimaye michango hiyo itagusa na hata kubadilisha mustakabali mzima wa maisha ya vijana/watoto wetu....na kuwafanya kufikia malengo na ndoto zao katika maisha.....hilo si jambo dogo!

    Nadhani tukiacha ushabiki Muheshimiwa kwa upande huu wa kuongoza harambee hasa za kuchangia maendeleo ya elimu yuko vizuri....anaonekana huyu bwana mkubwa anaweza kufanya harambee mahali popote nchini na akakusanya "fweza"....nayo huenda ikawa ni karama, eeh!?

    ReplyDelete
  2. Well said chief! Kubwa ni kwamba hii harambe ama hii kazi anayoifanya Mh. EL hatimaye itamnufaisha nani?? Je ni yeye mwenyewe? Je ni familia yake? Jibu ni jamii kwa ujumla tena jamii hii iliyopo na ijayo

    Anastahili pongezi na Mungu azidi kumpa nguvu katika haya ayafanyayo. Hongera sana Mhe. Edward N. Lowassa!

    ReplyDelete
  3. Hakika mheshimiwa huyu amejawa na hulka zote za uongozi-- he has leadership attributes and thats why people can follow him and be able to contribute for their own development!. he can tap the existing resources for the benefit of the society- thats a visionary leader who has conviction and charisma! These are the leaders we would like to maintain in this country! wish you the very best!

    ReplyDelete
  4. Usipompongeza huyu mheshimiwa una mtindio wa Ubongo. Natamani na Uraisi mumpe maana anaonekana kufaa kubeba jukumu hilo na atalimudu. Ni mtu ambae jamii inamkubali kwa ayatendayo ingawa wapo wachahce wenye mtazamo tofauti. Big up Lowassa and stay blessed

    ReplyDelete
  5. Job Job Job is the key for our country economy. I don't see anybody is talking about Job creation

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...