Na Abdulaziz video,Mwanza Mhariri mtendaji wa Kampuni ya New Habari Absalom Kibanda leo amekabidhiwa tuzo ya Uandishi wa kishujaa na Utumishi uliotukuka ya Marehemu Daud Mwangosi baada ya Mhariri huyo kukumbwa na tukio la uvamizi na kisha kutobolewa jicho na watu wasiofahamika Machi 6 mwaka huu. 
 Kabla ya makabidhiano ya tuzo hiyo wadau wote wa habari wakasimama na kisha kuimba wimbo maalumu wa kumuenzi Marehemu Daud Mwangosi. 
 Akizungumza na wadau wa habari Jijini Mwanza.
Baada ya makabidhiano hayo mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Tido Mhando amewahimiza waandishi wa habari kuendelea kupambana katika jitihada za kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa. 
 Kutokana na umuhimu wa tuzo hii ya Marehemu Daud Mwangosi aliyeuwawa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la machozi lililolipuliwa visivyo September 2 mwaka jana kijijini nyololo mkoani Iringa Mhando akatumia fursa hii kulaani vikali vitendo vya kuminya uhuru wa habari vinavyofanywa na baadhi ya viongozi nchini. 
 Baada ya kibanda kukabidhiwa tuzo hiyo pamoja na hundi ya shilingi millioni kumi akawapa moyo wa ujasiri waandishi wa habari kote nchi wa kutonyamazishwa wakati wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao licha ya kuwepo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo zikiwemo za vitisho.
 Kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya habari nchini wadau wa habari wakiwemo wakongwe katika fani hii hawakubaki nyuma kuelezea mitazamo yao kuhusu uelekeo wa sekta hii. Tuzo za uandishi wa kishujaa na utumishi uliotukuka ya Marehemu Daud Mwangosi itakuwa ikitolewa kila mwaka ili kutambua michango mbalimbali inayotolewa na waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao ya kikazi.
 Wadau wa habari aliohudhuria  hafla hiyo jijini Mwanza leo

Mgeni  rasmi katika hafla  hiyo ya kukabidhi tuzo ya Daudi Mwangosi Bw  Tido Mhando  wa tatu  kulia  akimkabidhi mshindi  mfano  wa hundi ya Tsh milioni 10  Absalom Kibanda tuzo  yenye  thamani ya Tsh  milioni 10,0000 katikati ni mjane  wa Mwangosi  Itika Mwangosi  wa kwanza  kushoto ni makamu wa rais wa UTPC Jane Mihanji na  rais  wake  Keneth Simbaya.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera sana Absalom kwa kutunukiwa tuzo na Million 10 za Mwangosi. Waandaaji natumaini mjane wa Daudi Mwangosi hapo naye mnamtunza maana mumewe ndiye alikuwa bread winner na kauliwa na askari alafu mnatoa million 10 kama tuzo ya mwanae kwa wengine wenye uwezo wao wakati yeye analia njaa.
    mdau josheffu dar.

    ReplyDelete
  2. Wanna hekima njema kuhusu mjane waheshimiwa hawa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...