Na Abdulaziz video,Mwanza Mhariri mtendaji wa Kampuni ya New Habari Absalom Kibanda leo
amekabidhiwa tuzo ya Uandishi wa kishujaa na Utumishi uliotukuka ya
Marehemu Daud Mwangosi baada ya Mhariri huyo kukumbwa na tukio la
uvamizi na kisha kutobolewa jicho na watu wasiofahamika Machi 6 mwaka
huu.
Kabla ya makabidhiano ya tuzo hiyo wadau wote wa habari wakasimama na
kisha kuimba wimbo maalumu wa kumuenzi Marehemu Daud Mwangosi.
Akizungumza na wadau wa habari Jijini Mwanza.
Baada ya makabidhiano
hayo mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Tido
Mhando amewahimiza waandishi wa habari kuendelea kupambana katika
jitihada za kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa.
Kutokana na umuhimu wa tuzo hii ya Marehemu Daud Mwangosi aliyeuwawa
kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la machozi lililolipuliwa
visivyo September 2 mwaka jana kijijini nyololo mkoani Iringa Mhando
akatumia fursa hii kulaani vikali vitendo vya kuminya uhuru wa habari
vinavyofanywa na baadhi ya viongozi nchini.
Baada ya kibanda kukabidhiwa tuzo hiyo pamoja na hundi ya shilingi
millioni kumi akawapa moyo wa ujasiri waandishi wa habari kote nchi wa
kutonyamazishwa wakati wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao licha ya
kuwepo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo zikiwemo za
vitisho.
Kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya habari nchini wadau wa habari wakiwemo wakongwe katika fani hii hawakubaki nyuma kuelezea mitazamo yao kuhusu uelekeo wa sekta hii. Tuzo za uandishi wa kishujaa na utumishi uliotukuka ya Marehemu Daud Mwangosi itakuwa ikitolewa kila mwaka ili kutambua michango mbalimbali inayotolewa na waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao ya kikazi.
Wadau wa habari aliohudhuria hafla hiyo jijini Mwanza leo


Hongera sana Absalom kwa kutunukiwa tuzo na Million 10 za Mwangosi. Waandaaji natumaini mjane wa Daudi Mwangosi hapo naye mnamtunza maana mumewe ndiye alikuwa bread winner na kauliwa na askari alafu mnatoa million 10 kama tuzo ya mwanae kwa wengine wenye uwezo wao wakati yeye analia njaa.
ReplyDeletemdau josheffu dar.
Wanna hekima njema kuhusu mjane waheshimiwa hawa
ReplyDelete