MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili nchini Kenya, Anastazia Mukabwa, aliyethibitisha kuwa miongoni mwa watakaotumbuiza katika Tamasha la Krismasi litakalorindima Dar es Salaam Desemba 25 mwaka huu, pia katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki.

Tamasha hilo la Krismasi limepangwa kusheheni waimbaji kochokocho wa nyimbo za Injili, miongoni mwao akiwamo mwimbaji huyo galacha wa nyimbo za Injili, Mukabwa.

Mukabwa anatoa mwito kwa watu kujitokeza kwa wingi ili 'wavue viatu' siku hiyo aliyopania kukonga nyoyo za mashabiki atakapopanda jukwaani katika tamasha hilo. Kulingana na taarifa yake iliyotolewa na waandaaji wa tamasha hilo, msanii huyo amepanga kuwapa mashabiki raha na kuwataka wake mkao wa kula wakisubiri vitu vyake.

“Nimejipanga, najua mashabiki wa Tanzania wanataka kitu gani, nitawapa raha, mambo ya Kuvua Viatu watayasikia na mengine, watafurahi sana. “Kwa vile Rose (Muhando) atakuwepo, nitashirikiana kwenye wimbo huo na nyimbo zangu mpya nitazitoa huko kwa mara ya kwanza, ni mambo mazuri yatakuwepo,” alitamba.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama alisema Mukabwa aliyeimba kwa kumshirikisha mwimbaji nguli wa Tanzania, Rose Muhando katika wimbo wa Vua Kiatu, ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...