Benki ya NMB inazidi kuwa karibu yako na sasa inakuletea akaunti mpya inayoitwa NMB Business Account Plus maalum kwa ajili ya wafanyabiashara.

NMB Business Account Plus ni akaunti inayoruhusu kutumia kadi ya ATM katika mashine za ATM zaidi ya 500 nchi nzima, kumwezesha mteja kupata huduma ya ‘overdraft’ kusaidia biashara yake kwenda vizuri, ina gharama nafuu za uendeshaji, inamwezesha kupata statimenti ya bure ya kila mwezi, kufungua akaunti kwa kiwango nafuu na aweze kupata huduma ya hundi inayotambulika na benki nyingine.

Akizungumza katika uzinduzi huo jijini Mwanza, Mkuu wa kitengo cha Bishara wa NMB, Filbert Mponzi alisema “NMB imekopesha wajasiriliamali zaidi ya 55,000 kupitia matawi yake zaidi ya 150 yaliotapakaa nchi nzima. hivyo basi, uzinduzi wa akaunti ya NMB Business Account Plus utawawezesha wafanyabiashara kutumia kadi za ATM, vitabu cha hundi pamoja na kufurahia huduma za NMB mobile”

Ili kufaidika na akaunti hii mpya kutoka NMB. Fungua NMB Business akaunti Plus leo.

Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Waziri Barnabas wakipeana mkono na mwenyekiti wa kituo cha biashara Mwanza (NMB Business Club) baada ya uzinduzi wa NMB Business Account Plus. wakishuhudia kutoka kulia ni Mkuu wa kitengo cha Bishara wa NMB, Filbert Mponzi na Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Straton Chilongola

Sehemu ya wafanyakazi wa NMB waliohudhuria uzinduzi huo uliofanyika katika kituo cha Biashara Mwanza (NMB Business Center) wakiwa katika picha ya pamoja.

Meneja Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa akimweleza jambo Meneja kituo cha biashara Mwanza (NMB Business Center), Mike Grata wakati wa uzinduzi wa NMB Business Account Plus

Sehemu ya wateja wa NMB waliohudhuria uzinduzi huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...