Mashabiki wa Simba na Yanga kwenye miji ya Tunduma na Morogoro nao watapata fursa ya kuburudika katika michezo mbalimbali kupitia bonanza maalum la Nani Mtani Jembe lililoandaliwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager litakalofanyika uwanja wa Mwaka mjini Tunduma na Kiwanja cha Ndege mjini Morogoro siku ya Jumapili wikendi hii.
Mratibu wa mabonanza hayo Lawrence Andrew, amesema kuwa michezo mbalimbali ikiwemo soka bonanza la wachezaji saba kila upande, kuvuta kamba, na pia mpira wa mezani maarufu kama fussball itapamba mabonanza hayo. Burudani mbalimbali pia zitapamba bonanza litakalofanyika Tunduma zikiwemo burudani ya muziki kutoka bendi ya High Class pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wa mkoani Mbeya.
Kwa Mkoa wa Morogoro bendi maarufu mkoani humo ya Beacon Sound itatoa burudani kabambe kwa mashabiki watakaojumuika kushiriki bonanza hilo huku wasanii wa kundi maarufu la dansi GYT wakilishambulia jukwaa vilivyo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...