Kamanda wa Kikosi cha Polisi Bandarini Zanzibar akiongoza Operesheni wa kukagua magunia yaliokuwa na Pembe za Tembo yaliokamatwa katika bandari hiyoleo yakiwa katika harakati ya kusafirishwa nje ya Nchi kupitia bandari hiyo, zoezi hilo limefanywa chini ya Jeshi la Polisi Bandari Kikosi cha KMKM, yalikuwa katika Kontena la futi 40.
Askari wa jeshi la Polisi wakitowa Pembe za Tembo katika makunia wakati wa zoezi hilo leo asubuhi katika bandari ya Malindi Zanzibar.
Magunia haya yakiwa na sehena na makombe ya pwani wakati katikati yakiwa na viroba vya mPembe za Tembo ambayo yakiwa yamehifadhiwa katika Kontena likiwa tayari kusafirishwa nje ya Nchi, limegunduliwa katika bandari ya Zanzibar leo asubuhi.
Zoezi likiendelea kupekuwa makunia ya Makombe ya Pwani kutowa magunia yaliohifadhiwa Pembe za Tembo
Baadhi ya Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari ya Malindi Zanzibar yakisubiri kuhisabiwa kupata idadi kamali na thamani yake na uzito kwa ujumla.
Operesheni ikiendelea kuhesabu Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari ya Zanzibar wakiweka hesabu sawa kuhakikisha hesabu iliokamilika na kupata thamani yake halisi.
Zikipimwa uzito kujuwa uzito wake kila gunia likipimwa kupata uzito wake wote.


Haya tena mtamtafuta mchawi na kuundwa kwa kamati tele za kuwajua wahusika wakati hilo contena lina documents zinazoonyesha linatoka wapi na linaenda wapi.
ReplyDeleteHayo meno ya tembo yataishia mifukoni mwa vigogo wa nchi.
Mawaziri,polisi,wabunge ,wakuu wa mikoa ,wilaya nk nk ndio watagawana na kesi kwisha.
Tuombe mungu .....mungu ibariki Danganyika
Ubalozi wa china umeahidi kuleta wachina 10,000 kila mwaka kama watalii.
ReplyDeleteIkiwa liko soko la uhakika la kuuza pembe/meno ya tembo huko duniani na kwamba hii peke yake ni kishawishi kikubwa kwa watu kujaribu kulifikia soko hilo, basi tunahitaji mikakati na sera madhubuti sana kunusuru kizazi cha tembo wetu!
ReplyDeleteLakini jingine ni kwamba lazima tkubali kuwa hakuna nia ya dhati hasa kwa upande wa matajiri wa nchi tajiri za huko soko liliko juu ya kunusuru tembo wetu; kwahiyo ikiwa serikali za nchi zetu hizi nazo hazitaonyesha nia ya dhati juu ya jambo hili kwa kutunga sera & sheria na kuzitekeleza kwa kumaanisha basi huko mbele tembo walio hai tutawaonaga tu kwenye "videos".....ni changamoto kubwa sana kwa serikali zetu katika Afrika, Tanzania ikiwa ni moja wapo!
Kwa Zanzibar Tembo walikuwa wakipatikana MAKUNDUCHI tu, tena enzi hizooooo kabla ya Mwaka kongwa (sherehe za kijadi za watu wa Makunduchi, wilaya ya kusini Unguja) haujahalalishwa. Baada ya kuja kwa mwaka kongwa na kuvamiwa na watu wa mjini, tembo wa Makunduchi nao wakaanza kuvamiwa.
ReplyDeleteSasa hii habari ya hizi pembe ndani ya Zanzibar sijui inakaaje. Watu wa bandari bubu za Sakura, Bagamoyo, na Mkokotoni itabidi hujibu hoja.
TANZANIA shamba la bibi. Inakuwaje dunia nzima ione TZ ni mahali pa dezo?
ReplyDeleteHapa kuna siri nzito.. Kagasheki kama Mwakyembe hajui anapambana na nani. Hawa wanaokamatwa ni vidagaa tu. Mapapa wanaachwa. Hii vita haiwezekani. Kagasheki weka silaha chini vita hutaiweza.
Watanzania tumekosa uzalendo. Wageni wanayumia hii tabia yetu ya uzalendoless kuhujumu uchumi. Makuu hapa wanahusika .mzee Kagasheki pole sana
ReplyDeleteWaingereza wanamsemo kwamba 'Sit back and watch'manake ukitaka kufuatilia huu "mpango mzima" wa ujangili unaweza kufa kwa ugongwa wa moyo.Hata hivyo mimi nahisi hii biashara haina tofauti na ya mihadharati kwa maana ya kwamba inahusisha watu WAZITO(untouchables).Naomba niishie hapa,naogopa,mikono imeanza kutetemeka!
ReplyDeleteDavid V
Nakubaliana na wewe David,hii ni biashara ya watu wakubwa na ndi maana unaona hata waandishi wanatetemeka.Kwa sababu report inasema kukamatwa kwa pembe za ndovu lakini hatutajiwi wahusika ama watuhumiwa,ina maana zimekamatwa peke yake,tulitegemea angalau tujue nani alikuwa anasafirisha hata kama anatumiwa na wazito.
ReplyDeleteHuu ni muendelezo wa zile zilizokamatwa mikocheni kwa wale china,.. JAMANI HAO WANAOKAMATWA NA HIZO SHEHENA WANYONGWE HADHARANI, NA WAUAJI PIA NA MAKULI WA MADAWA YA KULEVYA. HIvi tunaogopa nini kurekebisha hii sheria, kwani hao vigogo wataishi milele? huu ni upumbavu uliopindukia kuskia kila aina ya uhalifu eti kuna kigogo sijui ni nini? AGHHHH. WANYONGWE TU. HAKUNA HAJA YA KUWAPELEKA KUJAZA MAJELA YETU. KIKWETE HAKUNA KIGOGO ZAIDI YA WEWE NCHI HII, PLIZ SAINI KIFO KWA HAO MAKULI NA MATAJIRI WAO. TEMBO AKIBAKI MMOJA NCHI NAWE PIA UTALAUMIWA..Plz sain sheria ya kunyonga hawa wahalifuu
ReplyDeleteTalalila nyiiiiiiiiiiingi Tanzania debe tupu, kazi kuonea wananchi, wataisha kama walivoisha faru,mwizi hamtaji mwizi mwenzie.
ReplyDelete