Ua aina ya 'Poppy' linaloonekana
kuvaliwa na karibu kila mtu nchini Uingereza kwa sasa linasemekana lilianza
kuvaliwa tangu mwaka 1920 kukumbuka askari veterani waliokufa vitani.
Historia inasema ua hilo lilipata
umaarufu kutokana na shairi katika vita kuu ya kwanza liitwalo “In Flanders
Fields”, na wa kwanza kulitumia walikuwa askari veterani wa Marekani maarufu
kama American Legion, kukumbuka askari wa Marekani waliopoteza maisha katika
vita hiyo iliyopiganwa mwaka 1914-1918. Baadae askari wa zamani katika nchi za
Jumuiya ya Madola wakarithi utamaduni huo.
Hivi leo ua la Poppy linavaliwa
zaidi Uingereza na Canada kukumbuka askari wao waliopoteza maisha katika kila
aina ya vita tokea mwaka 1914. Aghalabu ua hilo huvaliwa siku ya Kumbukumbu ya
Mashujaa wa nchi hizo kila Novemba 11 na majuma kadhaa kabla ya siku hiyo.
Mashada ya maua ya Poppy pia huwekwa kwenye
makaburi ya mashujaa hao.
Uingereza ndio wanaoushabikia
sana utamaduni huu. Katika majuma kuelekea siku hiyo ya Novemba 11, maua hayo
yanagawiwa na chama cha maveterani wa vita wa Uingereza (The Royal British
Legion), ambapo hulipwa pesa chache kukisaida chama hicho.




ni ua linalowakumbusha wazee walio pigana vita vya pili
ReplyDeleteSasa mbona Picha na Habari havifanani?
ReplyDeleteHabari kuhusu Mauwa kuwakumbuka Mashujaa wa Vita, Picha Mchezaji Mpira wa Timu ya Liverpool!
Ahhh Mjomba Michuzi na Liverpool yako mwanawane!
ReplyDeleteIna maana Shujaa wa vita sasa hapa ndiyo Liverpool?