Ua aina ya 'Poppy' linaloonekana kuvaliwa na karibu kila mtu nchini Uingereza kwa sasa linasemekana lilianza kuvaliwa tangu mwaka 1920 kukumbuka askari veterani waliokufa vitani.
Historia inasema ua hilo lilipata umaarufu kutokana na shairi katika vita kuu ya kwanza liitwalo “In Flanders Fields”, na wa kwanza kulitumia walikuwa askari veterani wa Marekani maarufu kama American Legion, kukumbuka askari wa Marekani waliopoteza maisha katika vita hiyo iliyopiganwa mwaka 1914-1918. Baadae askari wa zamani katika nchi za Jumuiya ya Madola wakarithi utamaduni huo.
Hivi leo ua la Poppy linavaliwa zaidi Uingereza na Canada kukumbuka askari wao waliopoteza maisha katika kila aina ya vita tokea mwaka 1914. Aghalabu ua hilo huvaliwa siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa wa nchi hizo kila Novemba 11 na majuma kadhaa kabla ya siku hiyo. Mashada ya maua ya Poppy pia huwekwa kwenye  makaburi ya mashujaa hao.
Uingereza ndio wanaoushabikia sana utamaduni huu. Katika majuma kuelekea siku hiyo ya Novemba 11, maua hayo yanagawiwa na chama cha maveterani wa vita wa Uingereza (The Royal British Legion), ambapo hulipwa pesa chache kukisaida chama hicho. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. ni ua linalowakumbusha wazee walio pigana vita vya pili

    ReplyDelete
  2. Sasa mbona Picha na Habari havifanani?

    Habari kuhusu Mauwa kuwakumbuka Mashujaa wa Vita, Picha Mchezaji Mpira wa Timu ya Liverpool!

    ReplyDelete
  3. Ahhh Mjomba Michuzi na Liverpool yako mwanawane!

    Ina maana Shujaa wa vita sasa hapa ndiyo Liverpool?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...