Waziri wa Maji na umwagiliaji,Profesa,Jumanne Maghembe(kulia)akizungumza na Mkurugenzi wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi nchini(GEPF)Daudi Msangi(kushoto)walipokutana kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma mara baada ya bunge kupitisha muswada wa marekebisho ya mfuko wa(GEPF),katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko huo Joyce Shaidi.
Waziri wa Kazi Ajira na maendeleo ya Vijana,Gaudensia Kabaka(kushto)akijadiliana jambo na Mbunge wa Kigoma mjini CCM,Peter Serukamba(kulia)nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma,mara baada ya bunge kupitisha sheria ya marekebisho ya mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi nchini(GEPF)katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya kusimamia Mifuko ya hifadhi ya Jamii nchini,(SSRA) Irene Isaka
Waziri wa Habari Vijana utamaduni na michezo,Dk.Fenella Mukangara,(kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama, ambae pia ni mjumbe wa Bodi ya Baraza la sanaa Taifa (BASATA)walipokutana nje ya ukumbi was Bunge mjini Dodoma,(katikati)ni Mbunge wa Peramiho,CCM,Jenista Mhagama.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji,Francins Mtungi,(kulia)akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama(kushoto) Promotions,Alex Msama,walipokutana nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma mara baada ya Rais Kikwete kulihutubia Bunge(katikati)ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho,CCM,Jenista Mhagama.
Katibu Mkuu wa CCM,Abdurahman Kinana(kulia)akisalimiana na Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka.katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama,Promotions,Alex Msama walipokutana kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Naona matukio ya Alex Msama akiwa bungeni yameibuka tena na yeye anapokea posho za vikao bungeni nini?
ReplyDeleteHivi huyu Msama ni Mbunge wa Jimbo gani, maana kila tunapoambiwa matukio ya bungeni naye yumo, ama ndio 2015 maandalizi? au ofisi kahamishia bungeni, duh!
ReplyDelete