President Jakaya Mrisho Kikwete with President Jacob Zuma, President Yoweri Museveni and President Idriss Deby of Chad head for  the conference hall  on Tuesday night at the Oliver Tambo Centre in Pretoria, South Africa, to discuss with other African leaders the formation of a rapid-deployment emergency force to swiftly intervene in crises on the continent. STATE HOUSE PHOTOS. 
 President Jakaya Mrisho Kikwete walks towards the conference hall  with President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda on Tuesday night at the Oliver Tambo Centre in Pretoria, South Africa, to discuss with other African leaders the formation of a rapid-deployment emergency force to swiftly intervene in crises on the continent.
 President Jakaya Mrisho Kikwete consults with the Chief of Defence General Davis Mwamunyange and Ambassador rajabu Gamaha, Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Forein Affarirs and International Cooperation on Tuesday night at the Oliver Tambo Centre in Pretoria, South Africa, where discussions opened on  the formation of a rapid-deployment emergency force to swiftly intervene in crises on the continent.
President Jakaya Mrisho Kikwete and President Yoweri Kaguta Museveni  join other African leaders on  Tuesday night at the Oliver Tambo Centre in Pretoria, South Africa, to discuss the formation of a rapid-deployment emergency force to swiftly intervene in crises on the continent.

Tanzania kuchangia askari katika Kikosi cha Afrika

Tanzania ni miongoni mwa nchi tano za Afrika ambazo zimejitolea kutoa askari wa kuunda Kikosi cha Kukabiliana na Migogoro ya Kijeshi Barani Afrika cha African Capacity for Immediate Response to Crises (ACIRC) kitakachoundwa kwa mujibu wa uamuzi wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).
Tanzania itatoa kikosi kimoja (Battalion Group) na nchi nyingine ambazo zimekubali kuchangia askari ama polisi katika Kikosi hicho ni Afrika Kusini, Uganda, Algeria na Chad.
Nchi hizo zilijitokeza kushiriki katika Kikosi hicho wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Majeshi wa nchi hizo uliofanyika Jumapili iliyopita mjini Pretoria, Afrika Kusini, mkutano ambao maamuzi yake yameidhinishwa na kukubaliwa na wakuu wa nchi  akiwamo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Wakuu hao walikutana Pretoria jana, Jumanne, Novemba 5, 2013.
Uamuzi wa kuanzisha Kikosi hicho ulitolewa na Wakuu wa Nchi wanachama wa AU waliokutana katika kikao chao cha 22 cha kawaida mwezi Mei,  mwaka huu, 2013, mjini Addis Ababa.
ACIRC kitakuwa kikosi cha muda wakati Afrika inaendelea na maandalizi yake ya kuunda Jeshi la Kudumu la Afrika (Africa Standby Force) na Lenye Uwezo wa Kukabiliana na Migogoro Haraka na Popote (Rapid Deployment Force).
Jeshi hili litakuwa ni jeshi lenye uwezo wa kuingia nchi yoyote, chini ya AU, na hivyo wakati mwingine litatumika kutuliza migogoro katika nchi yoyote ya Afrika hata kama nchi husika haijaomba msaada wa jeshi hilo.
Jeshi hilo litakalofanya kazi yake chini ya mfumo wa Amani na Usalama katika Afrika – African Peace and Security Architecture (APSA) litaiwezesha AU kuwa na jeshi la askari na polisi wenye uwezo na nguvu kukabiliana na mizozo ya kijeshi barani humo na kuwa vifaa vyake vitatolewa nchi wanachama wa AU ambao watakuwa tayari kushiriki katika mpango huo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
6 Novemba, 2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Vikao vya kuzungumzia Majeshi na Usimamizi wa Amani ktk Afrika, ni Pigo kwa Maraisi wawili wa 'Coaliion of willing' ,Yule Mzee wa Uganda na Yule Kijana asiyezeeka na kukua kiakili wa Rwanda!!!

    Kwa kutahayari kijana asiyezeeka wa Jijini Kigali amekwepa kufika Mkutanoni amemtuma Louise Mushikiwabo Waziri wa Mambo ya nje.!

    Majeshi yake ya Mgambo ya Msituni yamefyekwa vibaya sana na Majeshi ya UN-Tanzania Brigade, hadi wamesalimu amri na kushusha bunduki chini...chezea Tanzania weye?

    Ni aibu kisi gani?

    ReplyDelete
  2. Kaguta Museveni na wenzako Uhuru Kenyatta na Paul Kagame,

    Itawagharimu sana na kuumia sana mioyoni mwenu kwa Kupaa kwa Tanzania mliyokuwa mkiishusha na kuidharau na sasa mnajikuta mkiionea wivu,,,UTHIBITISHO NI VIKAO VYETU VYA KUITENGA TANZANIA,,,(Coalition of willing).

    Kama ilivyo andikwa ktk Vitabu vya Mungu kuhusu ISRAEL NA KUJALIWA KWAKE KUWA TAIFA TEULE, mkumbuke na pia ya kuwa MABAKI YA MTU WA KALE YAMEPATIKANA OLDUVAI GORGE KTK HII HII TANZANIA MLIYOIDHARAU KABLA HII NI WAZI YA KUWA MATAIFA TEULE SIYO ISRAEL PEKEE NA PIA IMO TANZANIA !!!

    ReplyDelete
  3. Hahahahaha!

    Raisi Kikwete anatoa tabasamu na kicheko cha Ushindi !


    Kikwete anacheka Kitaalamu hapo anaonana na M-7 ni vile ameshinda vita kwa Majeshi yake UN-Tanzania Brigade kuyatwanga na kuyachakaza vikali Majeshi ya Ushirika ya Museveni na Kagame ya M-23 hadi Kagame amejisikia aibu kuja Mkutanoni!!!

    Kagame aibu na Majeshi yake ya Msituni, Mkutanoni Pretoria anatuma kuwakilishwa na Waziri wake wa Kike wa Mambo ya nje.

    Aibu !

    Ahhh jamani kushindwa kubaya ?

    ReplyDelete
  4. Museveni picha ya kwanza anamwangalia Kikwete kwa jicho la 'jino pembe' inaonekana wazi amekoma !

    Majeshi yenu ya Msituni M-23 wewe na Kagame yamechapwa vibaya sana na UN-Tanzania Brigade hadi yamesalimu amri na kusimamisha vita kwa kukubali amani!!!

    Weweeeee chezea Tanzania weye?, mpelekee Salamu Kagame aliyekwepa kuhudhuria Mkutano Afrika Kusini mweleze umeonana ana kwa ana na Simba wa Afrika JAKAYA MRISHO KIKWETE, MTOTO WA JULIUS KAMBARAGE NYERERE, DUME LA MBEGU, MTAMBO WA CHUMA MWANZO MWISHO!

    ReplyDelete
  5. Raisi Paul Kagame yupo wapi?

    Ameshindwa kufika Mkutanoni Afrika Kusini kwa sababu hizi tatu (3) chini:

    1.Anasikia aibu baada ya kushindwa Vita na Tanzania UN-Brigade Kundi lake la M-23.

    2.Alijua kama angefika ni lazima angekutana na Jakaya Kikwete uso kwa uso kwa mara ya Pili (tena akiwa ameshindwa Vita Msituni) baada ya mara ya kwanza kuonana naye Kampala-Uganda akiwa na matumaini ktk maendeleo ya Vita huko nyuma msituni...na sasa ,amenyong'onyea na amevunjika moyo kabisa!

    3.Yupo Msituni Mpakani na Congo-DRC akiyakaribisha na kuyapokea Majeshi yake ya M-23 na kwa kuyafariji kwa kuyapa pole baada ya Kushindwa Vita na Tanzania UN-Brigade!

    Dr.Kikwete alikupa Ushauri mzuri sana uongee na Waasi mmalize tofauti zenu wewe ukakasirika!

    ReplyDelete
  6. Kalagabaho m-7 Mnafiki sana anachangia majeshi ya kujinyoa ndevu. Mnafiki wanametupokonya EA wazo la mwalimu RIP.Hawatafika popote

    ReplyDelete
  7. Kaguta kama anabubujikwa na jasho vile

    ReplyDelete
  8. Mdau wa 7 juu ...Kaguta kama anabubujika na jasho vile.

    Ndio hivyo kwa kuwa wamejikakamua Kuunda Muungano WA NCHI ZAO 3 ndai ya Muungasno kamili wa nchi 5 wa awali na sasa KAMASI ZINAWATOKA MIPANGO WALIYOWEKA HATA FEDHA ZA MIRADI HAWANA HUKU GHARAMA ZIKIPARAMA ZAIDI YA BAJETI ZAO!!!
    ...................................
    MIRADI YAO YA MIOUNDO MBINU WALIYOKALIA VIKAO KUITENGA TANZANIA HAITEKELEZEKI, HUKU WAKIWA HAWA KOPESHEKI NAM PIA KUKATIWA MISAADA YA NJE NA WAHISANI!
    ...................................

    Hicho ndicho kinachomtoa majasho hapo huyo KAGUTA!

    ReplyDelete
  9. 'Coalition of willing' wana wkati mgumu sana kwa sasa.

    1.Majeshi yao ya Ushirikiano Msituni M-23 (ambyo yalikuwa ni ATM ya Dolla za MAREKANI kwa kuwaingizia mapato ama SACCOS kwa wizi wa Madini ya Congo-DRC) yameshindwa vibaya sana na kusalimu amri baada ya Kipigo cha Kijeshi cha DIRECT COMBACT kutoka kwa Majemedari wa Kijeshi wa Tanzania ktk UN-Brigade.

    2.Kaguta amekatiwa Misaada na Wahisani, Uhuru ana Kesi ICC imemkalia vibya, Kagame nyota yake imefifia Dunia nzima imemgeuka analaumiwa sana kwa kushiriki vita na Kusaidia Majambazi wa vita.

    3.Kuamka na kupaa kwa Tanzania ktk kila eneo ni msiba mkubwa sana kwao, kinyume na walivyotarajia.

    -SEKTA YA UTALII TANZANIA INAZIDI KUPAA.

    -DIPLOMASIA ZA KIMATAIFA TANZANIA INAZIDI KUPAA KILELENI, ANGALIENI HAWA JAMAA WA K3 WAMEHUDHURIA VIKO VINGAPI NJE MWAKA HUU ZAIDI YA MKUTANO WA 68 WA UN NEW YORK MWEZI SEPTEMBA?, NI KUWA KWA SASA HAWAKUBALIKI KIMATAIFA!.

    -SEKTA NA NISHATI NDIO USIPIME MWANZO MWISHO!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...