DMK, Alex Kassuwi na Davis Mosha
wakisubiri mwili wa Martha Julius Nyerere
International Airport October 30, 2013
Ndugu zangu hadi hivi sasa siamini yaliyotokea, bado haijaingia akilini kama mke wangu mpenzi
Martha Shani hatunaye tena! Siamini kama Martha amefariki! Naona yupo. Ndugu zangu kwa sasa nipo katika kipindi kigumu sana, nikiwa mwenyewe nikiangalia watoto machozi yanitoka. Maneno ya kinywa changu hayawezi kuelezea kuugua kwa nafsi na roho yangu.
Ndugu zangu, |Mama zangu, kaka zangu, dada zangu, mashemeji zangu, wakwe zangu, marafiki na jamaa zangu pamoja na yote haya sina budi kutoa shukrani zangu kwa yote mliyonitendea kuanzia maombi hospitali, kuwa nasi kipindi chote cha msiba mpaka kuusafirisha na kuuhifadhi mwili wa mpenzi wangu nyumbani Tanzania ambapo tulizika Alhamis Oktoba 31,2013 huko Puma Singida.
SHUKRANI ZA PEKEE KWA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI
Mhe. Balozi Liberata Mulamula,
Balozi wa Tanzania nchini Marekani.
Natoa shukrani za pekee kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa kuwezesha makaratasi ya kuusafirisha mwili wa mpenzi mke wangu.
Shukrani kwa wafanyakazi wote wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa kutununulia tiketi tatu za ndege, mimi na watoto wangu wawili.
Shukrani za pekee kwa Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Familia yake, kwa kuwa nasi kuanzia siku ya msiba hadi mwisho, na kuwahamasisha watanzania wote bila kujali dini,itikadi za kisiasa wala ukabila.


wafiwa poleni sana na Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu na ailiwaze familia nzima na kuipa Amani yake
ReplyDelete