Wadau naomba kuuliza historia ya kundi hili na lilikuwa lina comprise akina nani na nani na je bado bado liko au la na je wanapata royalties?

Inaonekana kuna jamaa wanasema kuwa hili kundi ni la Kenya lakini wengine wanasema ni la Tanzania je tofauti yao na Ikhwan Safaa ya Zanzibar ni nini?

Je RTD wanalo duka au website ambayo tunaweza kununua hizi nyimbo online? Na kwa nini wanamziki wa siku hizi hawaimbi kama hawa?

Mdau,
Barking. London, UK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Egyptian Musical Club lilikuwa ni Kundi liko Dar es Salaam tangu napata akili katika Miaka ya mapema ya 1960's.
    Tuwasiliane soka@sokainbongo.com nakufanyia utafiti kidogo.
    Ila nina hakika RTD wanazo Nyimbo zake na pia wanazo details za Musicians wa Bendi hiyo.

    ReplyDelete
  2. Ndugu yangu na jirani yangu hapa Barking. Huu wimbo sio wa Kenya. Kikundi hichi ni Cha Zanzibar ingawa hakikuwa na uhai mrefu. Wimbo huu uliimbwa zamani sana na ili kuthibitisha kuwa wimbo huu si wa Kenya wala Pwani ya Tanga angalia upigaji wao. Kama utasikiliza tarabu za Kenya za Zuhura Swalehe utaona kuwa mpigo wao wa taarabu una ladha za chakacha au ladha za nachi ya kihindi. Hii ni tafauti hai kabisa ya tannzu za upigaji wa taarabu za Pwani ya Afrika Mashariki. Ukisikiliza taarabu za Tanga, zinafanana sana zile za Kenya kwa mapigo. Mpigo huu wa Taarabu ambao unajumuisha vifaa vingi kama vile ganun, udi, figla, harmoni na rika ni maarufu sana kule Misri na ndio hasa mfumo wa taarabu ya asili ya Zanzibar. Mpigo huu kwa sasa unapigwa na kikundi cha Malindi na kikundi cha taarab cha Taifa ambacho ni mchanganyiko wa vikundi tafauti vya taarab hapa kwetu. Kama sikosei mwimbaju huyu ameshafariki na anaitwa Abbas Mzee (Kumradhi kama sikumpatia) siku zishakuwa nyingi.
    Mdau kwa maelezo zaidi tuonane hapa Barking. Nipigie simu 07438442036

    ReplyDelete
  3. Mdau wa Egyptian kuna baadhi ya mambo ambayo nayafahamu kuhusu hii club ambayo zamani kwenye kipindi cha taarabu cha RTD tulikuwa tunasikiliza nyimbo zao. Nyimbo zao zilikuwa na mantiki na mafunzo mengi mazuri.

    Nyimbo zao maarufu ninazozikumbuka ni hiyo Yatima na Harusi.

    Mmoja wa watungaji/waimbaji alikuwa anaitwa Abbas Mzee.

    Hili ni kundi la Tz original hamna ukenya hapo. Makao yao makuu yalikuwa ni Dar.

    Ni tofauti na Ikhwan Safaa ya Malindi Zanzibar ambayo mpaka leo bado ipo.

    Waimbaji wa siku hizi ni fedha tu na mipasho kwa kwenda mbele, mafunzo ni machache sana.

    ReplyDelete
  4. hili ni kunid la Taznia bara makazi yao ilikuwa dar es salaam na hawa jammaa waliwahi kutumbuiza alipokuja rais wa misri sina uhakika hiii ni stori nilipewa na marahemu baba yangu kuwa kundi hili lili perform mbele ya raisi Gamal abdul nasiri na vombo walivyotumia vilikuwa hafifu na hivyo raisi huyo aliahidi kuwaletea vyombo na ala zote za muziki wa taarab ndipo kundi hili likaendelea na muziki na kutoa nyimbo kadhaa ikiwamo yatima na nyingine nyingi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...