Taifa Stars sasa inacheza na Zimbabwe mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date itakayofanyika keshokutwa Jumanne (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Awali Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa icheze na Kenya (Harambee Stars), lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) lilituma taarifa jana jioni (Novemba 16 mwaka huu) likieleza kuwa timu yake haitacheza tena mechi hiyo.

Kikosi cha Zimbabwe chenye msafara wa watu 30 kinatarajia kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kesho (saa 3 asubuhi) tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 11 kamili jioni.

Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Uganda wakati Kamishna atakuwa Leslie Liunda wa Dar es Salaam. Mwamuzi wa mezani ni Oden Mbaga pia wa Dar es Salaam.

Stars chini ya Kocha Kim Poulsen ipo kambini tangu Novemba 12 mwaka huu kujiwinda kwa mechi hiyo. Kim amejumuisha kwenye kikosi chake wachezaji watano wanaocheza mpira wa miguu nje ya Tanzania.
…5,000/- NDIYO KIINGILIO CHA KUISHANGILIA STARS.

Kiingilio katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya wenyeji Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe ni sh. 5,000 wakati tiketi zitaanza kuuzwa Jumatatu (Novemba 18 mwaka huu) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Mbali ya kiingilio hicho cha sh. 5,000 ambacho ni kwa viti vya bluu na kijani, viingilio vingine ni sh. 30,000 kwa VIP A, sh. 20,000 kwa VIP B, sh. 15,000 kwa VIP C wakati viti vya rangi ya chungwa ni sh. 10,000.

Tiketi zitauzwa katika magari maalumu katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, Sokoni Kariakoo, Dar Live Mbagala, OilCom Ubungo, BMM Salon iliyopo Sinza Madukani, Uwanja wa Uhuru, mgahawa wa Brake Point uliopo Kijitonyama, na kituo cha mafuta Buguruni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Viingilio vikubwa MECHI YA KAWAIDA TFF INAJIKOSESHA MAPATO FANYA UWANJA WOTE 3000,. VIP A30000 B C 10000 NA MECHI ITANGAZE SANA IANZE Sa 12 mtashangaa mapato

    ReplyDelete
  2. Mechi YA KAWAIDA SANA VIINGILIO VIKUBWA,A B C WEKA VIKUBWA MJIUMIZE WAKUBWA LAKINI KWA WANAZI HASWA AMBAO PESA SHIDA ILA NDO WAPENZI WA UKWELI FANYA UWANJA WOTE 3000 PESA ITAKUWA NYINGI AJABU , TANGAZA SANA MECHI IAANZE SAA 12 VINGINEVYO TFF MNAJIHUJUMU ANAYEBISHA ANIPIGHE BAADA YA MECHI KUHUSU MAHUDHURIO NA MAPATO KAMA HAKUNA MABADILILO YA VIINGILIO

    ReplyDelete
  3. TFF hawajihujumu makusudi bali uwezo wao wakufikiri ndipo ulipokomea, hawakugombea uongozi kwa ajili ya kuendeleza mpira bali kula kwa ulafi kupitia mpira.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...