Taifa Stars sasa inacheza na Zimbabwe mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date itakayofanyika keshokutwa Jumanne (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Awali Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa icheze na Kenya (Harambee Stars), lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) lilituma taarifa jana jioni (Novemba 16 mwaka huu) likieleza kuwa timu yake haitacheza tena mechi hiyo.
Kikosi cha Zimbabwe chenye msafara wa watu 30 kinatarajia kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kesho (saa 3 asubuhi) tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 11 kamili jioni.
Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Uganda wakati Kamishna atakuwa Leslie Liunda wa Dar es Salaam. Mwamuzi wa mezani ni Oden Mbaga pia wa Dar es Salaam.
Stars chini ya Kocha Kim Poulsen ipo kambini tangu Novemba 12 mwaka huu kujiwinda kwa mechi hiyo. Kim amejumuisha kwenye kikosi chake wachezaji watano wanaocheza mpira wa miguu nje ya Tanzania.
…5,000/- NDIYO KIINGILIO CHA KUISHANGILIA STARS.
Kiingilio katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya wenyeji Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe ni sh. 5,000 wakati tiketi zitaanza kuuzwa Jumatatu (Novemba 18 mwaka huu) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Mbali ya kiingilio hicho cha sh. 5,000 ambacho ni kwa viti vya bluu na kijani, viingilio vingine ni sh. 30,000 kwa VIP A, sh. 20,000 kwa VIP B, sh. 15,000 kwa VIP C wakati viti vya rangi ya chungwa ni sh. 10,000.
Tiketi zitauzwa katika magari maalumu katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, Sokoni Kariakoo, Dar Live Mbagala, OilCom Ubungo, BMM Salon iliyopo Sinza Madukani, Uwanja wa Uhuru, mgahawa wa Brake Point uliopo Kijitonyama, na kituo cha mafuta Buguruni.
Viingilio vikubwa MECHI YA KAWAIDA TFF INAJIKOSESHA MAPATO FANYA UWANJA WOTE 3000,. VIP A30000 B C 10000 NA MECHI ITANGAZE SANA IANZE Sa 12 mtashangaa mapato
ReplyDeleteMechi YA KAWAIDA SANA VIINGILIO VIKUBWA,A B C WEKA VIKUBWA MJIUMIZE WAKUBWA LAKINI KWA WANAZI HASWA AMBAO PESA SHIDA ILA NDO WAPENZI WA UKWELI FANYA UWANJA WOTE 3000 PESA ITAKUWA NYINGI AJABU , TANGAZA SANA MECHI IAANZE SAA 12 VINGINEVYO TFF MNAJIHUJUMU ANAYEBISHA ANIPIGHE BAADA YA MECHI KUHUSU MAHUDHURIO NA MAPATO KAMA HAKUNA MABADILILO YA VIINGILIO
ReplyDeleteTFF hawajihujumu makusudi bali uwezo wao wakufikiri ndipo ulipokomea, hawakugombea uongozi kwa ajili ya kuendeleza mpira bali kula kwa ulafi kupitia mpira.
ReplyDelete