MAANDALIZI ya tamasha kubwa la filamu lijulikanalo kwa jina la Arusha African Film Festival yanaendelea vizuri na kila kitu kinaenda kama kilivyopangwa, tamasha hilo ambalo linategemegea kuonyesha zaidi ya filamu 70 kutoka nchi 20, litambatana na utoaji wa semina ya utengenezaji wa filamu kwa watengeneza filamu ambao watajisajili kwa ajili ya Semina hiyo ambayo ni muhimu sana kwa watayarishaji na tasnia ya filamu kwa ujumla.

Akiongea na FC mmoja wa waratibu wa tamasha hilo Mary Birdi amesema kuwa ni tamasha ambalo linaleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya filamu Swahiliwood, kwani watengeneza filamu kutoka sehemu mbalimbali watafika na kubadilisha mawazo na watengezaji wa filamu wa Tanzania, ni muhimu kila mdau akajipanga na kushiriki tamasha hili linalojenga.

“Ni tamasha ambalo linajenga tasnia ya filamu nchini hasa pale watu wetu wanavyopata workshop kwa ajili ya kazi wanazofanya, siku hizi teknorojia inakwenda kwa kasi ni vema kupata shortcourse mara kwa mara, lakini ni nafasi pia ya kutangaza Utalii wetu,”anasema Mary.

Tamasha la AAFF litazinduliwa tarehe 29.November.2013 Mount Meru Hotel Jijini Arusha wakati Semina sitaanza rasmi tarehe 25.

November. 2013 sambamba na maonyesho ya filamu katika sehemu zifutazo Alliance Francaise, Via Via, Mount Meru Hotel, Mango Tree, na New Arusha Hotel tamasha hili kiingilio ni bure kabisa, Siku 7 USIKOSE KUSHUHUDIA FILAMU KALI KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...