Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi wa kijiji cha Kilangawani kufuatia malalamiko yao kwa Serikali juu ya Opersheni Tokomeza. Wengi wao walikiri kutegemea hifadhi ya akiba ya Uwanda kulisha mifugo yao.
Jambo ambalo wafugaji wameiomba Serikali kuwatafutia maeneo mbadala ya ufugaji. Kwa upande wao wakulima wameiomba Serikali kuharakisha kutafuta suluhu ya mifugo inayozagaa vijijini na mashambani baada ya kufukuzwa kwenye hifadhi kabla ya msimu wa mvua unaokaribia kuanza kwa ajili ya kilimo kuepusha migogoro kati yao na wafugaji.
Wavuvi na Wajasiliamali wa samaki waliokuwa wakifanya shughuli zao katika ziwa Rukwa nao wameiomba Serikali iwape muda wa kuvua angalao wa miezi mitatu ili waweze kurudisha madeni ya mikopo kutoka taasisi za fedha walizokopa na kupata nauli za kurudi makwao kwani wengi wao wametoka maeneo tofauti ya mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Njombe na Kilimanjaro.
Sehemu ya kundi kubwa la Ng'ombe likionekana mitaani kutafuta malisho na maji katika kijiji cha Maleza katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa baada ya kufukuzwa katika hifadhi ya akiba ya Uwanda (Uwanda Game Reserve) ikiwa ni matokeo ya operesheni Tokomeza inayofanywa na Serikali kunusuru mali asili nchini.
Maeneo yaliyoathirika kutokana na Operesheni Tokomeza yapo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ambapo zoezi la kuwaondoa majangili na wavamizi wa hifadhi za misitu limegusa vijiji saba (7) vya Ilambo, Maleza, Kilangawana, Mkusi, Kilyamatundu, Nankanga na Msila. Pia wananchi wanaoishi pembezoni mwa Ziwa Rukwa ambapo jumla ya kambi 13 za wavuvi zimechomwa moto.
Inakadiriwa kuwa takribani watu 1600 wameathiriwa na zoezi hili. Aidha, yapo makundi makubwa ya mifugo (ng’ombe) ambayo yamezagaa vijijini na kuna uhaba mkubwa wa chakula kwa familia hizo kutokana na nyumba zao na vyakula kuchomwa moto.HABARI NA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Serikali ya Tanzania iache siasa make kila mmoja anaangalia usawa wake kwa wananchi.Hifadhi ni muhimu kwa Taifa na dunia nzima.Wabunge wanaokuja juu wanatetea eneo dogo lao bila kujali matokeo ya athari za maumivu ya mabadiriko hewa ni wakati muafaka serikali kuanza kubadilrsha mitazamo ya kiufugaji tanzania ama tutakwisha kwa jangwa.
ReplyDeleteMm naiunga mkono hiyo tokomeza,,mm nalipenda sn JESHI LANGU LA JWTZ maana hawana mchezo hatakidogo wanapotekeleza majukumu yao safisheni ili hifadhi zetu ziludi kama enzi ya J K NYERERE (RIP) baba wa taifa,,nashangaa hao wabunge wanao ilalamikia hiyo tokomeza,,kwa mtazamo wangu wao ndio bure kabisa maana wao wapowapo tu hawajui nn maana ya mipangilio ya majimboni mwao,,wengi wao toka wachaguliwe maisha yao DAR na DODOMA,,tuliangalieni hili swala kwenye Katiba mpya,kila mbunge aishi kwenye jimbo lake na Dodoma ahudhulie vikao tu vya bunge akimaliza aludi kwenye jimbo lake,,mfano mdogo kwa wadau wote, HIVI UTAJUAJE FAMILIA YAKO KAMA WANAMATATIZO WAKATI WEWE MWENYEWE HULALI NDANI YA NYUMBA YAKO?,,,naitwa mdudu kakakuona nipo huku UINGEREZA,,nawapendeni wote huko hasa JWTZ because they know what,anaejua amalizie n hp mtanielewa vyema.
ReplyDeleteMimi huwa nashangaa sana Tanzania na watanzania.Ivi kuna faida gani ya kurundika mifugo yote hiyoo,nina hakika ukifanya utafiti wa kutathmini idadi ya watanzania wanaokunywa maziwa ya ngombe au kutumia nyama ya ngombe sidhani kama itaendana na idadi hiyo ya mifugo iliyotapakaa kila pande ya nchi.Athari kubwa inakuja mbele yetu .
ReplyDelete