Afisa Afya Mratibu wa Kampeni ya Usafi wa Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Severin Tarimo akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mkoa wa Iringa kuhusu maadhimisho ya siku ya kunawa mikono,siku ya matumizi ya choo duniani na wiki ya usafi Tanzania inayotekelezwa katika mkakati wa taifa wa kampeni ya usafi  iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa mkoani Iringa mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya waandishi habari mkoa wa Iringa wakimsikiliza Afisa Afya Mratibu wa Kampeni ya Usafi wa Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Severin Tarimo (hayupo pichani) kuhusu maadhimisho ya siku ya kunawa mikono,siku ya matumizi ya choo duniani na wiki ya usafi Tanzania inayotekelezwa katika mkakati wa taifa wa kampeni ya usafi  iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa
mkoani (picha zote na Denis Mlowe)

WATAKIWA KUNAWA MIKONO KABLA YA KULA KUJIKINGA MAGONJWA
MLIPUKO

Na Denis Mlowe,Iringa

JAMII imeshauriwa kuchukua tahadhari kwa kunawa mikono kabla na baada ya kula sambamba na kutumia vyoo bora ili kuweza kujikinga na maambukizi ya maradhi ya kuharisha na kutapika.

Ushauri huo umetolewa na Afisa Afya Mratibu wa Kampeni ya Usafi wa Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Severin Tarimo wakati akizungumza na wanahabari wa mkoa wa Iringa kuhusu maadhimisho ya siku ya kunawa mikono,siku ya matumizi ya choo duniani na wiki ya usafi Tanzania inayotekelezwa katika mkakati wa taifa wa kampeni ya usafi  iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa
mkoani hapa.

Alisema maradhi ya kuharisha bado yanaendelea katika maeneo
mbalimbali ya mkoa wa Iringa hivyo jamii inapaswa kuchukua tahadhari ya 
kujikinga na maaradhi hayo ya kuambukiza kwa kutumia vyoo bora na kunawa 
mikono.

“Tafiti zilizofanyika zimegundua kutokunawa mikono vizuri
kabla ya kula chakula, baada ya kutoka chooni, wakati wowote kama umeshika kitu  
ambacho kinaweza kuleta madhara na kutokuwa na matumizi sahihi ya choo  
kunachangia zaidi ya asilimia 80 ya magonjwa ya kuambukiza kama kuhara, minyoo  
na maralia” alisema Tarimo

Tarimo alisema utafiti unaonesha kuwa kunawa mikono pekee kunapunguza
uwezekano wa kupata maambukizi ya maradhi ya kuharisha kwa Asilimia 50 na hivyo   
kuitaka jamii isipuuzie tabia hiyo ya kunawa mikono kabla na baada ya kula.

Alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuhamasisha jamii
kuhusu umuhimu wa tabia za usafi binafsi na usafi wa mazingira katika kulinda   
na kuboresha afya hivyo kila jamii inapaswa kujenga vyoo bora kwa wasio na  
vyoo, kuboresha vyoo duni au vibovu na kuweka maji ya kunawa mikono kwa sabuni.

Alitoa wito kwa shule zote ziwafundishe wanafunzi jinsi ya
kutengeneza kibuyu chirizi na waweke karibu na vyoo vya shule wavitumie na  
kuendeleza elimu hiyo katika mazingira wanayoishi.

Katika tafiti hiyo imebaini kata ya Nduli ni moja ya kata
zilizopo katika kampeni ya usafi kitaifa zilizo na asilimia ndogo ya kaya zenye 
vyoo bora na sehemu ya kunawa mikono.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwanini Marekani watu wengi hawanawi mikono kabla ya kula chakula lakini hawaugui magonjwa ya milipuko???????????????????. Sijawahi kusikia watu wanaugua kipindupindu hata siku moja. Wadau naomba majibu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...