Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk Sengondo Mvungi, Mjumbe wa
Tume ya Katiba.
Waziri Nchimbi alisema upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa
zaidi ya asilimia 80 ambapo tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na
mapanga na simu moja ya mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika
mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
jijini Dar es Salaam leo.
Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na
waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na
uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine.
Kushoto ni Naibu Waziri
wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kulia ni Kamishna wa Polisi Kanda Maalum
Dar es Salaam, Suleiman Kova.
Naelewa kuwa matatizo yetu ni mengi na uwezo wa vifaa vya dola ni mdogo. Hata hivyo, ningependa ku-propose kuwepo kwa camera za usalama ktk sehemu mbali mbali jijini na miji mingine. Pia labda na sie wenyewe wananchi mbali ya kuweka fences tuweke CCTVs ambazo zinaweza kusaidia wakati wa matokeo kama haya na mengine pia. Am I a dreamer?
ReplyDeleteBlackmpingo
Hapa sasa ndio mara zooote Mamlaka za Kiusalama zinapo tutega!!!
ReplyDeleteSasa kwa uchache kwa nini msitoe ORODHA ya Majina yao ikiwezekana na Picha?
Iaweza kuwa sisi Wanahchi tukawa na mchango zaidi ktk harakati hizi.
Hahahaha!
ReplyDeleteAfande Kova hapo amekaa kama anataka kusimama vile?
Anakaa kama yupo 'stand by' hivi.
Sasa je Wahalifu walikuwa wawindaji wa mafao 'kama Vibaka waporaji tu' ama walikusudia kumfanyia?
ReplyDeleteHivi Mtu akikutwa nyumbaani kwake na panga au simu ni kosa? mbona vitu hivi vimejaa madukani na ukitaka kununua huulizwi kitu chochote.
ReplyDelete