Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk Sengondo Mvungi, Mjumbe wa Tume ya Katiba. 
Waziri Nchimbi alisema upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. 
Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. 
Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kulia ni Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Naelewa kuwa matatizo yetu ni mengi na uwezo wa vifaa vya dola ni mdogo. Hata hivyo, ningependa ku-propose kuwepo kwa camera za usalama ktk sehemu mbali mbali jijini na miji mingine. Pia labda na sie wenyewe wananchi mbali ya kuweka fences tuweke CCTVs ambazo zinaweza kusaidia wakati wa matokeo kama haya na mengine pia. Am I a dreamer?
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  2. Hapa sasa ndio mara zooote Mamlaka za Kiusalama zinapo tutega!!!

    Sasa kwa uchache kwa nini msitoe ORODHA ya Majina yao ikiwezekana na Picha?

    Iaweza kuwa sisi Wanahchi tukawa na mchango zaidi ktk harakati hizi.

    ReplyDelete
  3. Hahahaha!

    Afande Kova hapo amekaa kama anataka kusimama vile?

    Anakaa kama yupo 'stand by' hivi.

    ReplyDelete
  4. Sasa je Wahalifu walikuwa wawindaji wa mafao 'kama Vibaka waporaji tu' ama walikusudia kumfanyia?

    ReplyDelete
  5. Hivi Mtu akikutwa nyumbaani kwake na panga au simu ni kosa? mbona vitu hivi vimejaa madukani na ukitaka kununua huulizwi kitu chochote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...