Bondia Alibaba Ramadhani wa mkoani Kilimanjaro (shoto) akizungumza na Dixon
Busagaga wa globu ya jamii Moshi muda mfupi kabla ya kuanza safari ya
kuelekea jijini Dar es salaam jana kwa ajili ya pambano lake dhidi ya
Bondia Japhet Kaseba litakalo fanyika kesho.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
BONDIA Alibaba Ramadhani wa mkoani Kilimanjaro ametamba kumpiga kwa
Knock out (KO) bondia Japheth Kaseba wa jijini Dar es Salaam.
Alibaba alitoa kauli hiyo jana muda mfupi kabla ya kupanda gari
kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya shughuli ya kupima afya na
uzito itakayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Friends Corner leo saa
4 kuelekea mpambano wao wa kesho.
Akizungumza kwa kujiamini Alibaba amesema amaefanya maandalizi ya
kutosha na yuko tayari kuwashangazza mashabiki wa mchezo huo watako
jitokeza katika kushuhudia mpambano huo hiyo kesho.
Pambano hilo linalofanyika kwa uratibu Ibrahim Kamwe wa Kampuni ya
Bigright Promotions ya Dar es Salaam kwa kivuli cha PST,
litasindikizwa na mengine sita likiwemo la Karage Suba na Fadhili
Awadh ‘Tiger’ katika uzani wa welter kg 66 watakaozichapa kwa raundi
kumi.
Akizungumzia pambano hilo la kesho, Kamwe amesema wengine watakaopima
uzito leo ni Mbarouk Heri atakayezichapa dhidi ya Lusekelo Daudi na
Issa Omar Nampepeche ataoneshana kazi na Hassan Kiwale ‘Moro Best.’
Naye Zumba Kukwe atazichapa na Jacob Maganga; Adam Yahya vs Harman
Shekivuli, Jocky Hamis v Mbena Rajab, Ernest Bujiku na Shah Kasim,
Shaban Kitongoji v Mwinyi Mzengela, Shaban Manjoly v Kassim Chuma.
Aidha, bondia mwingine wa Tanzania anayeishi nchini Canada, Kareem
Kutch, atacheza na Tata Boy kwa pambano la kimataifa la Kickboxing la
raund tano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...