Bondia Lulu Kayage kushoto aki oneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hamisi Belege wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya Ilala Kayage anajiandaa na mpambano wake na Mariam Abdallah utakaofanyika Desemba 25 katika ukumbi wa friends corner hotel wakisindikiza mpambano wa Mohamed Matumla na Nassibu Ramadhani 
Bondia Lulu Kayage kushoto aki oneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hamisi Belege wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya Ilala Kayage anajiandaa na mpambano wake na Mariam Abdallah utakaofanyika Desemba 25 katika ukumbi wa friends corner hotel wakisindikiza mpambano wa Mohamed Matumla na Nassibu Ramadhani.

Picha na Habari na  Super D
Akizungumzia mpambano huo Lulu Kayage amesema kuwa: "Mimi nafanya mazoezi mwaka mzima niwe na mechi niwe sina mechi. Hivyo nipo fiti wakati wowote kucheza mpambano huo kwani mimi kwa sasa ndie nataraji kuwa bingwa kwa upande wa wanawake.

"Hivyo wanawake wanaoweza kuhimili vishindo vya mchezo wa masumbwi wajitokeze ili kuleta changamoto ya mchezo huo unaopendwa na watu wengi duniani wakiwemo wanawake.

"Unajua mimi naiga staili ya Leila Ali ambaye alikuwa bingwa wa mchezo wa masumbwi duniani na mpaka sasa amestaafu bado ana heshimika hivyo nataka nifate nyayo zake hivyo naomba mashabiki wengi wajitokeze waje kutuunga mkono na kututia moyo wa kuendelea kuupenda mchezo wa masumbwi", Alisema Lulu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...