Waziri wa ujenzi John Pombe Magufuli akitoa salamu za rambirambi kwenye ibada ya mazishi ya aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza na Diwani wa kata ya Kisesa hadi mauti yalipomkuta Marehemu Clement Mabina.

Waziri wa ujenzi John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa familia ya Marehemu Mabina.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akito salamu za rambirambi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kwenye ibada ya mazishi ya Mabina.
Akitoa salamu za rambirambi kwaniaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarsti Ndikilo amesema kuwa, Rais Kikwete ametoa pole kwa wananchi wa Kisesa na Mkoa wa Mwanza juu ya tukio hili la msiba wa marehemu Mabina (58) na mtoto Tevery Malemi (12) kutokana na vifo vilivyosababishwa na mgogoro wa ardhi.
Ameongeza kuwa migogoro ya ardhi inapaswa kushughulikiwa kwa uangalifu mkubwa huku hekima na busara zikitumika kushughulikia utatuzi wa migogoro hiyo badala ya kutumia hasira jambo ambalo siku zote husababisha majonzi na madhara makubwa kwa jamii.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Steven Wasira akitoa salamu za rambirambi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nimefurahi kusikia kauli ya Mheshimiwa Rais akiongelea kiini cha tatizo sual la rdi. Na mimi naongeza ardhi ni suala nyeti sana. Kwa wafuatiliaji wa mambo wanaweza kujua nchi kama za Amerika ya kusini kuna movements za landless....mtaji wa masikini ni ardhi; sasa na yenyewe ikiwa ni ya kugombania inakuwa hatari sana.

    Nadhani umefika muda wa kulitafutia ufumbuzi ili suala ili kuepuka madhara makubwa zaidi siku za usoni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...