Na: Sylvester Onesmo 
wa Jeshi la Polisi Dodoma
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la JOYCE EMMANUEL maarufu kwa jina la SIIJIA mwenye umri wa miaka 33,  mkaazi wa Kijiji cha Godegode Wilayani Mpwapwa akiwa anajishughulisha na biashara haramu na kukamatwa na kete 650 za bangi, mbegu za bangi gm 600, bangi ambayo haijafungwa gm 350 na pombe ya moshi lita 2 na nusu. 
 Akiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwakwe Kaimu Kamanda Mkoa wa Dodoma ACP – SUZAN S. KAGANDA amesema uchunguzi wa awali unaonyesha mtuhumiwa huwa anasafirisha bidhaa hizo kutoka Wilayani Mpwapwa mpaka Mkoa jirani wa Morogoro ambako ndiko anauza biashara hiyo.Amesema  mtuhumiwa atapelekwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika. 
 Kamanda KAGANDA amesema Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Mkoani humo limefanya msako tarehe 10/12/2013 katika kijiji cha Isinghu Tarafa ya Mpwapwa Mjini Wilaya ya Mpwapwa katika nyumba ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la ZAMOYONI S/O MANYELEZI mwenye umri wa miaka 26, mgogo, mkulima, mkazi wa Kijiji cha Isinghu na kufanikiwa kukamata bunduki aina ya Gobole lisilokuwa na namba alilokuwa akimiliki kinyume cha sheria.  Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili mara baada ya upelelezi kukamilika. 
 Aidha Kamanda KAGANDA amesema katika msako unaoendeshwa na Jeshi la Polisi huko eneo la Kiboriani Wilayani Mpwapwa amekamatwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la GOSTON MGIRE mwenye miaka 28, mkulima, mmasai akiwa anajishughulisha na kilimo cha bangi. Polisi walifanya upekuzi shambani humo na kukuta shamba la ukubwa wa robo heka likiwa limelimwa bangi na kuliharibu. Mtuhumiwa ambaye ni mmiliki wa shamba hilo anashikiliwa na Jeshi la Polisi na atafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika.
 Msako unaendelea kufanyika maeneo mbalimbali hasa wakati huu wa kuelekea mwisho wa mwaka na sikukuu ya X-Mass. 
 Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi na jamii kwa ushirikiano wa kutupatia taarifa zinazofanikisha kukamatwa wahalifu. Tunatoa rai kwa wakazi wa Mjini Dodoma kuwa waangalifu na kuzingatia utii wa sheria bila shuruti, hususani katika kipindi hiki kuelekea sikukuu na mwaka mpya.
Kamanda Kaganda akionesha kwa wanahabari gobole lililokamatwa Mpwapwa
Juu na chini Kamanda Kaganda akionesha shehena ya bangi na mbegu za zao hilo haramu zilizokamatwa

Sehemu ya shehena ya bangi na mbegu za zao hilo haramu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hii kitu bangi balaa sana,mimi sivuti wala sijavuta bangi lakini nafikiri madhara ya bangi ni machache sana ukilinganisha na madhara ya sigara na pombe.Lakini pombe na sigara zaruhusiwa na karibu serikali zote duniani. Leo nimesoma kuwa Uruguay has become the first country in the world to make it legal to grow, sell and consume marijuana. Jambo moja wazi ni kwamba members of drug cartels will have to look for a job.

    ReplyDelete
  2. Bangi mbona kidogo!!

    ReplyDelete
  3. Me kwakweli nashangaa sana jeshi la polisi linajitangaza kwa kukamata bangi,wakati kuna uhalifu mkubwa zaidi ya huo watu wanaua tembo,wanauza madawa ya kulevya lakini wala hawakamtwi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...