Karibu katika sehemu ya pili ya kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production. Katika kipindi hiki, tunaendeleza mjadala juu KWANINI WANANDOA HUTEMBEA NJE YA NDOA? Wachangiaji studio walikuwa ni Elizabeth Cherehani, Denzel Musumba na Mubelwa Bandio
KARIBU UUNGANE NASI


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. The root cause ama chanzo cha mwanandoa kutoka nje ya ndoa,kwa mawazo yangu na hii ni kwa mwanandoa yeyote awe mwanamke au mwanamume, sababu kubwa ya kutoka nje ya ndoa ni tabia iliyo damuni ya ufuska tu ambayo mtu alikuwa nayo hata kabla ya kuamua kuingia katika ndoa.

    Watu wa namna hii, wanapoamua kuoa ama kuolewa hiyo tabia ya ufuska inawekwa dormant, ama inalala kwa muda, na mara unapotokea msukosuko kidogo, ama mabadiliko mbalimbali katika ndoa ambayo haiepukiki(i.e kuongezeka familia, kuzeeka, kufilisika, kupata utajiri, kugombana etc), tabia hii ya ufuska hurudi kwa nguvu kubwa kama suluhisho la matatizo yaliyopo.
    Tuwe wakweli tulioko kwenye ndoa, maisha ya ndoa hayawezi kubaki pale pale, kama siku ile mliyooana. Siku zinaenda, umri unaenda, mabadiliko ya kimwili yanatokea, priorities zinaongezeka na hasa family inapoongezeka, sasa baba ama mama anaeangalia uhalisi wa hali iliyopo, hawezi ku-ignore hili. Matatizo pia yanakuwepo. How to solve these include better communication and understanding in both parties, and being ready for a give and take compromise. Saa ingine ni bora kukubali yaishe tu, kama tofauti hazikubaliki. Lakini wote wanatakiwa tayari kuplay that part. Na isiwe upande mmoja tu peke yake.

    Mtu ambaye hakuwa na tabia ya ufuska ( i.e tamaa ya kutembea na watu tofauti tofauti kwa wakati mmoja, ama kubadilisha partners bila mpangilio), ni ngumu sana kutembea nje ya ndoa. Sana sana atamua kujiondoa katika hiyo ndoa na kuamua kutafuta mtu mwengine, lakini baada ya kuondoka katika ndoa hiyo.

    Kwa hivyo nionavyo hizo sababu zinazotolewa katika mada hii kuwa huenda ndio zinasababisha mtu kwenda nje ya ndoa ni symptoms tu ama cosmestics tu za underlying problem ambayo ni TABIA YA UFUSKA ambayo mtu alikuwa nayo looong before hajaingia katika ndoa.

    ReplyDelete
  2. The root cause ama chanzo cha mwanandoa kutoka nje ya ndoa NI NDOA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...