Waziri wa Uchukuzi,Dr Harisoni Mwakembe afanya ukakuguzi wa tiketi ilikubaini mabasi yaliyo toza gharama kubwa za nauli zakusafiria katika kipindi cha Xmass na mwaka mpya,badhi ya mabasi yalikamatwa nakuamuliwa kurudisha nauli zilizozidi abiria wao.zoezi hilo limefanyika majira ya alfajiri katika eneo la Visiga mkoani pwani na kila basi lilozidisha nauli lilitozwa faini ya shilingi laki mbili na nusu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hongera sana Mhe. Dr.Harrison Mwakyembe kwa Kazi iliyotukuka ya kuwaibukia hao Wahujumu Afajiri ya Majogoo kuwika!

    Ni kawaida yao hao wadau wa Usafiri wa Mabasi ya Mikoani kuwatoa damu abiria katika misimu kama huu wa Krismasi na Mwaka Mpya.

    WEMBE NI ULE ULE TUWANYOE MAFISADI KUANZIA NGAZI YA USAFIRI WA MABASI HADI NGAZI YA TAIFA!!!

    ReplyDelete
  2. Mwakyembeeeeeeee Ni mwanaume wa ukweeeli na kiongoooozi wa ukweeeli anatetea haki za wana nchi kupitaaaaa kiasi jamani!!!! Mungu mbariki muheshimiwa Mwakyembe Kila siku,

    ReplyDelete
  3. Tusiwe na tabia ya kulaumu wale "mizigo" tu, na hawa wanao onekana wanajitahidi tuwasifie.

    ReplyDelete
  4. Wajanja hao jamaa unafikiri wanaandika walichokutoza?

    ReplyDelete
  5. Huyu mh wala si mzigo hata siku moja, anafaa apewe nafasi. Ya Urais anawapenda wananchi wenzake. Mchapakazi

    ReplyDelete
  6. Safi sana jembe letu Mwakyembe
    Ila njoo na uku Arusha
    Nauli ya Arusha Moshi ni shilingi 6000 badala ya 3000

    ReplyDelete
  7. Kazi nzuri sana, Hon. Mwakyembe...watanzania wanataka kuona viongozi wetu kama hivyo unavyofanya wewe....yaani mkishughulikia moja kwa moja kero zinazo wanyanyasa wananchi.

    Unapoacha ofisi yenye "furu kiyoyozi" ukaenda field, na watu wakaona optput ya hicho unachokifanya huko ndiyo kuwajibika, Muheshimiwa...ndo uzalendo huo, baba!

    Ingawa hivyo, naamini "Waziri Mkubwa" hawezi kukupiga stop kama alivyomfanyizia Hon. J.P. Magufuli.

    ReplyDelete
  8. Lol hii kali waziri afanya kazi ya traffic!

    ReplyDelete
  9. Mwakyembe ni Jembe, Muheshimiwa mkuu wa Kaya usituondolee hili Jembe katika pangua pangua yako utakayofanya hivi karibuni, tupo chini ya miguu yako mkuu wa kaya

    ReplyDelete
  10. Sasa waziri atafanya kazi ngapi? Hakuna wasaidizi wake au polici wanao weza kufanya hiyo kazi.

    ReplyDelete
  11. Hivi mbona hotels na airlines zinaongeza bei kwenye high season lakini hazifuatiliwi. Gii sio ndio high season ya mabasi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...