![]() |
| Tony Baretto |
Na Muhidin Issa Michuzi
Nilikuwa nje ya Dar es salaam kikazi siku
ya Jumanne wakati Catherine-Rose, binti yake, aliponipigia simu na
kunifahamisha habari hii ya kustua na kusikitisha.
Lakini simu yake ilikuwa ni
moja ya nyingi nilizopokea siku hii zikiwa na
habari hizi za kustusha.
Ya kwanza ilitoka kwa rafiki yetu Mukesh
Josh, aliyeanza kwa kunipa pole, mapema asubuhi. Nilipomuuliza ya nini,
akashangaa kwa kusema huna habari kuwa rafiki yako Anthony Baretto amefariki dunia?
Kabla ya mwangwi wa habari hiyo iliyoufanya
moyo wangu unyong’onyee kutwa nzima kwa huzuni haujatuama, simu ya pili ikaita.
Hii ilikuwa inatoka Arusha kwa rafiki yetu mwingine Sukhdev Chattbar .
Alinipigia kutaka kuthibitisha habari hiyo. Tulilia kwa pamoja
nilipomthibitishia kwamba ni kweli Braza Tony is no more…
Kwa hali ya kawaida, na kama Mola
asingemchukua miaka mine iliyopita kwa ajali ya gari, ni wazi simu ingine ingetoka kwa kaka Hamidu Bisanga (aliyekuwa mmoja wa Brotherhood yetu mie, Tony, Suk Chat, Mkumbwa Ally, Jajis Merali na Danfold Mpumilwa a.k.a Dan Lutte). Lakini simu
ya nne, ya tano na nyingine nyingi ziliendelea kunimiminikia kutoka kila kona, kwani
wengi walijua urafiki wangu na Tony na familia yake.
Si urafiki tu, bali pia undugu wa karibu,
tangia najiunga na Tanzania Standard Newspaper (TSN) wachapaji wa magazeti ya serikali ya Daily News na Sunday News January 1, 1990.
Yeye Tony, Mzee Wenceslaus Mushi, Isaac
Mruma, Charles Kizigha, Vicent Urio (RiP) Ernest Millinga (RiP), Jonas Marios, Jonas Mwasumbi, Chattbar, Bisanga (RiP), Reggie Mhango (RiP), Charles
Rajabu, Mkumbwa Ali, Attilio Tagalile,
Willie Chiwango, Adam Lusekelo (RiP) Khadija Riyami, Emmanuel Bulugu (RiP), Mzee Mdimi, Bob
Karashani, Stephen Rweikiza, Rose Kalemera, Ichikaeli Maro, Pudenciana Temba, Joyce Mhaville, Halima Shariff, Chemi Che-Mponda, Mzee Boniface Byarugaba ndio walionipokea Daily News kwa mikono miwili na kuwa
mwanga wangu mkuu wa kunionesha njia sahihi lakini iliyojaa kona na mabonde na
gharika ya tasnia hii adhimu ya habari.
Nadiriki kusema Tony na wote
hao niliowataja kuwa ndio walionitaga, walionilea na kunifikisha hapa padogo nilipo
kitaaluma. Sijui nifanye nini ama niseme kitu gani kuwalipa fadhira hiyo.
Ni vigumu kuamini kwamba Tony, aliyekuwa
Mkuu wa Kitengo cha Matangazo cha Tanzania Standard Newspapers (TSN) wachapaji
wa magazeti ya serikali ya Daily News na Sunday News, hatunaye tena. Utendaji kazi wake uliojaa utani na ucheshi wakati wowote, uwe wa matatizo ama fanaka, ulikuwa
hauna mfanowe.
Nakumbuka siku moja wafanyakazi wa Daily
News tulipofika kazini pale mtaa wa Maktaba jijini Dar es salaam asubuhi moja na kukuta milango imetiwa
kufuli na mwenye nyumba wetu (Printpak) kutokana na kutolipa pango. Hakuna
aliyeamini kuwa pamoja na kufungiwa nje, gazeti la siku ya pili yake lingetoka
kama kawaida, kwani kila kitu kilikuwa kimefungiwa ndani.
Lakini siyo Tony. Hata kabla ya saa tatu haijatimia tayari yeye na Reggie Mhango walishafungua ofisi chini ya mti pembezoni mwa jengo la ofisi yetu, baada ya kumuomba muuza kahawa na kashata nafasi katika meza yake pale. Wakaongoza mapambano ya kutengeneza gazeti kwa ushujaa ambao sintousahau.
Lakini siyo Tony. Hata kabla ya saa tatu haijatimia tayari yeye na Reggie Mhango walishafungua ofisi chini ya mti pembezoni mwa jengo la ofisi yetu, baada ya kumuomba muuza kahawa na kashata nafasi katika meza yake pale. Wakaongoza mapambano ya kutengeneza gazeti kwa ushujaa ambao sintousahau.
Na
kweli, kesho yake Daily News lilikuwa mitaani kama kawaida. Vinginevyo kwa mara ya kwanza katika historia yake ya miaka 75 wakati huo, gazeti hilo lisingeona
mwaka wa jua!
Huyo ndiyo alikuwa Tony
Baretto.
Ni kweli kwamba mtu anapoaga dunia ndiyo
watu humtaja kwa maneno ya sifa na uzuri wake wakati alipokuwa hai, lakini si
uwongo kwamba Tony alikuwa si mtu wa kawaida, na aliyestahili sifa zote hizo na
za ziada. Nembo zake kuu tatu – Upara,
macho makubwa nyuma ya miwani na madevu (kama ya gaidi, tulimtania, naye
alicheka tu) hazitosahaulika kwa sie tuliofanya naye kazi na pia kuwa karibu
kifamilia.
Buriani kaka yangu, ndugu yangu, mshauri wangu na mwanafamilia
wangu Anthony Baretto. Eelewa kuwa huko
ulikotangulia, ambako sote tutafuata kwa muda tofauti, hatutakusahau milele.
Mke wako Pearl, na watoto wako Catherine-Rose na John-Paul tutalia nao na
kusherehekea pamoja maisha yako yaliyojaa bashasha na mapenzi kwa binadamu
wenzio.
SISI TULIKUPENDA, ILA MOLA KAKUPENDA
ZAIDI
NA AIWEKE ROHO YAKO MAHALI PEMA PEPONI



Ankal! You are a natural story teller. Je umeshafikiria kuandika vitabu? Kwa jinsi ulivyotiririka na kunifanya nijione niko hapo nawe katika msiba huu, nahisi iko haya ya kumuenzi Tony Baretto kwa kuwa mwandishi wa vitabu. You are a natural I tell you. Just sit down and jot down the lines! You are our Hammod Innes, Sheldon and the rest. I can smell it miles away..
ReplyDeleteMdau Canada
Ankal, pole sana kwa msiba uliokupata wewe na hiyo timu nzima.
ReplyDeleteHivi Ankal wewe unapolia sura yako inakuwaje? Naomba picha yako unapolia tafadhali. Bwana ametoa na Bwana huyo huyo amechukua. Jina lake ni kubwa sana.
Hamim Liverpool~New Albany, Ohio.
poleni jamani! tupole sote. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe
ReplyDeletendugu pole na msiba wa rafikio ambae ni kama ndugu,umefanya vema kuwataarifu watu kwa njia ya mtandao na kueleza yote ulio eleza ni wachache mno huweza kuwaenzi rafiki au aliemsaidia, huwa akifa huyo mtu basi waliobaki watoto na mkewe wanasahaulika nimeona alipofariki baba mzazi, alipokuwa hai marafiki na ndugu wengi aliowasaidia walimwita baba, alipofariki kila kitu tuliachiwa tubebe wenyewe,Mungu akuzidishie kuwakumbuka na kuchukua msiba kama wako.
ReplyDeleteBinafsi nimepokea taarifa za kifo cha Bareto kwa mstuko mkubwa kwani nilimfahamu kama mtu mchapakazi na mwenye weledi uliotukuka katika majukumu aliyokuwa akiyafanya na kuyasimamia.Ucheshi na uchangamfu wake ni jambo ambalo litawaliza wengi.Ametangulia,nasi tuko safarini.Mungu akupe mapumziko ya milele, amina.(Songoro Mnyonge)
ReplyDeleteMichizi,
ReplyDeleteKweli naungana na mdau wa kwanza kuhusu suala la kuandika kitabu. Umetoka mbali sana Michu na una mengi ya kuandika. Umeona nchi yetu tangia enzi za chama kimoja, magazei ya serikali mpaka leo ambako its a whole different ball game. I hope utafikiria suala la kuandika kitabu.
R.I.P Tony.
Mdau
Nimeumia sana kusikia kuwa Tony Baretto amefariki dunia. Yaani those good old days of Daily News Mimi nilianza pale 1984, na Tony alikuwa ananipa advice nzuri kuhusu maisha. May he rest in eternal peace. Amen. He will be missed.
ReplyDeleteWadau mnaotoa rai Michuzi aandike kitabu nawaunga mkono, sio tu kwa kuona mengi toka enzi hizo, bali pia uwezo wake wa kuelezea jambo kifasaha na lugha nyepesi lakini sio ya kitoto. Ankal Michuzi lifikirie hilo kwa manufaa ya sasa na ya baadaye. Watu kama wewe ni adimu nchi hii...Yaani toka walipotoweka kina Elvis Musiba, Eddy Ganzel, Hammie Rajab, Faraji Katalambula na wengineo wewe unaweza kabisa kuvaa viatu vyao...
ReplyDeleteDuuh Michizi ni kweli unaandika story vizuri sana ingawa ni msiba lakini ina raha kusoma na kuvuta mtu uendelee kusoma...pole sana na msiba wa huyo ndg yako..RIP Tonny. Ankal Michuzi Group unaweza kufungua /kuandika vitabu vya story pia maana naona una ka ujuzi/kipaji kaa hio kitu....
ReplyDeleteMdau wa Oxy
Mungu ailaze roho yamarehemu mahali pema peponi ameen.
ReplyDeleteWadau nami nawaunga mkono. Michuzi aandike vitabu. Mimi niliwahi kumshauri aanze na kitabu cha Photograph. " Tanzania in Picture" miaka kama minne iliyopita lakini bado hajaifanyia kazi. Wakati ule sikujuwa kama Ankal anaweza kuchoronga hadithi nzuri namna hii zenye uasilia. Ankal usipoteze kipaji hiki bure. Tayari unavitabu viwili jaza kalamu wino au chonga hiyo penseli kazi ianze. Nakutakia kila la kheri na poleni na msiba wa Tony. Tumempoteza Mtanzania Mzalendo.
ReplyDeletePoleni sana familia ya Baretto,Michuzi,jamaa na marafiki wengine.Umeandika vizuri Ankal,hata mimi nilyekuwa simfahamu,amenigusa.RIP Tonny.
ReplyDeleteSuala la Michuzi kuandika kitabu ni wazo zuri ila binafsi nachelea(I am afraid)na suala zima la soko,watanzania wengi wa kizazi hiki hatupendi kusoma vitabu.Ni suala la kufanyia utafiti wa hali ya juu.Lifanyie kazi Ankal-HE WHO HESITATES IS LOST.
David V
Really. Tony is of the ages. What a loss. He was a great friend when I worked with him. Banyan I used to call him, much as he was not one.
ReplyDeleteTony worked in advertising and many a times he would come over to Editorial to ask me look at some copies and do a re-write. He was quite hard self motivated chap whose bald was iconic to the display of the advertising pages.
Even when I left the Daily News, I still worked with him because my new employer was ad erasing quite a lot and sometimes we would need to put a notice for something after the pages are closed.
And even when again he too left he Daily News we continued th e association and did a few ads with his own company, by then in partnership with my friend Mikidad Mahamoud, the legendary radio broadcaster turned politician.
And socially, Tony was everywhere charming people and if you never met him at a party, you should know how good he was with charanga.
It is so sad I am not around there to celebrate his promotion to glory, but let all the family know that our sympathies are with them and as a catholic, the Prayers too.
Go and rest in Eternal Peace ANTHONY BARRETO
Pole sana Ankal kwa msiba huu ambao baada ya kusoma buriani yako nimeguswa na kuona si tuu wewe na familia mmepoteza ndugu yenu , na marafiki wamepoteza kipenzi chao bali na hata Taifa la Tanzania limepoteza Mzalendo asiye kifani. Kwa lugha ya kikerewe Tony Baretto alikuwa ni mmoja wa wale "unsung heroes " yaani watu ambao.wanafanya mambo makubwa na ya ajabu ili kukamilisha jambo lenye manufaa kwa wengi lakini ni wachache wanafahamu mchango.wao. kitendo.cha kukosa gazeti la kila siku mtaani tena enzi hizo ambazo hata magazeni za.udaku kulikuwa hamna ili kujipoza nayo kwa kweli hilo.lilikuwa Janga la Taifa.
ReplyDeleteNimekusoma nami naungana nawe ktk huzuni yako hii kwani baada ya kukusoma ni kama vile nimemfahamu Tony Baretto, ndugu.yako, rafiki yako.
..gaidi wako. Poleni sana wafiwa
Kwa hakika sote ni waja wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.
RIP Baretto
Mariam Mungula.UK
Wengi tumeshtushwa sana na kifo cha "mtu wa watu" Tony Bareto.
ReplyDeleteMay he endlessly rest in eternal peace. Amen.(David Kyungu)
Ankal, Ahsante kwa kumbukumbu hii. Mimi binafsi nina kijitabu kidogo cha kuwekea business card alichonipa Tony siku moja kabla sijaondoka Dar kuja Marekani kwa masomo. Juu kimeandikwa "Someone in Tanzania Loves Me." Only Tony could come up with such a lasting thought.
ReplyDeleteMwamoyo Hamza