Mwaka 2013 umefikia ukomo. Barani Afrika, mengi yametokea na mengine yanaendelea kutokea.
Mathalani kifo cha Mzee Madiba na mzozo unaoendelea Sudan Kusini na kufanya wanadiplomasia kuendelea kukuna vichwa vyao kila uchao kupata suluhu ya kudumu za mzozo huo ndani ya taifa hilo changa lililopaswa kuwa mfano.
Je nini mustakhbali wa Afrika baada ya Mandela? Na vipi Sudan Kusini?. Assumpta Massoi wa Idhaa hii alifanya mahojiano kwa njia ya simu na Mwanadiplomasia wa muda mrefu Katibu Mkuu Mstaafu wa uliokuwa Umoja wa nchi huru za Afrika, OAU sasa AU Dokta Salim Ahmed Salim kuhusu masuala hayo.
Kusikiliza mahojiano hayo bofya hapa.
Kama alivyo sema Balozi Dkt. Salim Ahmed Salim Mapungufu ya sifa za Uongozi kwa Viongozi wengi Afrika kinachopelekea Mustakabali tete UGONJWA WA RAISI SALVA KIIR WA SUDANI YA KUSINI NI ''UKABILA NA UFISADI KTK UONGOZI WAKE'' DHIDI YA MPINZANI WAKE DKT. MACHAR
ReplyDeleteTatizo lingine Raisi wa Sudani ya Kusini Salva Kiir anapata Ushauri mbaya kutoka kwa kundi la kukosa la akina K3 na ''Coalition of the Willing'' yao.
ReplyDeleteAngekuwa kwenye Kundi la akina K-SUCCESS yaani Rais Kikwete(Tanzania), Kabila (Congo-DRC)na Nkurunzinza(Burundi) yasingemfika yote hayo!!!
Ya Mungu ni makubwa sana!
ReplyDeleteHatuwaombei mabaya South Sudan, isipokuwa Kundi la CoW yaani ''Coaltion of the Willing'' walikuwa wanaichukulia South Sudan kama ndiyo itakayo jaza pengo la Tanzania baada ya kuitenga Tanzania, na sasa Mwenyezi Mungu ndio anatoa Maamuzi yake kwa kuiingiza nchi hiyo waliyo itegemea kwenye Maafa!
Tunafundishwa tusiwe na Nia mbaya mioyoni mwetu ni vile hiyo kitu hupewa Majibu mabaya papo kwa papo na Mungu kwa kuwa Mwenyezi Mungu kamwe hakatiwi denge!
Shame on you Kagame, Kaguta M-7 and Kenyatta!!!
Tanzania ilikuwa na Akili sana kuikataa Sudan ya Kusini ktk kupewa haraka Uanachama Jumuiya ya Afrika ya Mashariki !!!
ReplyDeleteHuku Kenya, Uganda na Rwanda zikishabikia na kuharakisha kuipa Uanachama.
Jamani hizi haraka haraka za Kenya, Uganda na Rwanda ktk mambo ya Afrika ya Mashariki madhara yake ndio kama hayo, mfano nchi hii tungeipa Uanachama moja kwa moja ingetuletea mzigo mkubwa na maafa kwetu!!!