Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya (sherry party) aliyowaandalia wake wa mabalozi wa nchi za nje walioko hapa nchini. Sherehe hiyo ilifanyika Ikulu tarehe 23.1.2014.
Kiongozi wa Umoja wa wake wa mabalozi waliopo hapa Tanzania Mama Celine Mpango, (ambaye ni Mke wa Balozi Juma Mpango wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) akitoa salamu zake kwa niaba ya wanajumuia hiyo wakati wa sherehe hiyo iliyofanyika Ikulu Trahe 23.1.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mume wa Balozi wa Zambia hapa nchini Bwana Victor Nsemiwe wakati wa sherry party aliyowaandalia wake wa mabalozi wa nchi za nje walioko hapa Tanzania. Sherehe hiyo ilifanyika Ikulu tarehe 23.01.2014.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. hahaha, sasa hii inabidi muitafutie jina mbadala maana hapa spouse wa Zambia ni mwanaume na shughuli kwa kiswahili mmesema ni ya wake wa mabalozi.

    ReplyDelete
  2. Sherehe ilikuwa kwa Wake wa Mabalozi, hii njemba ilikuwa isikuwepo. Mimi nilitaka kujua mume wa Rais kwa kiingereza anaitwaje?

    ReplyDelete
  3. Hii ni Sherry Party inayoandaliwa na mke wa rais wa nchi na hufanywa mwanzoni wa mwaka mpya. Sherehe hii ni kwa ajili ya wenza wa mabalozi wanaowakilisha nchi zao. Balozi akiwa ni mume, mke ndiye anaehudhuria. Na balozi akiwa ni mke, mume ndiye anaehudhuria.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...