Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza katika tafrija aliyoiandaa kwa wananchi wake na wageni mbalimbali ya kuukaribisha mwaka mpya 2014,iliyofanyika jana nyumbani kwake Ngarashi Monduli.Pembeni yake ni mkewe mama Regina Lowassa.

Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wageni waalikwa waliofika kwenye tafrija hiyo aliyoiandaa kwa wananchi wake na wageni mbalimbali ya kuukaribisha mwaka mpya 2014,iliyofanyika jana nyumbani kwake Ngarashi Monduli.
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) akizungumza na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mh. Goodluck Ole-Medeye wakati wa tafrija hiyo iliyofanyika jana nyumbani kwake Ngarashi Monduli. 

Wageni waalikwa mbalimbali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. barikiwa saana, ila naona ni watu wazito wazito tu, yatima na wasio na uwezo walikuwepo?

    ReplyDelete
  2. Mh. Lowasa 'alistaafu' uwaziri lini na wapi?

    ReplyDelete
  3. Hakuwahi kustaafu ila alilazimika kuacha kazi kwa kosa la kuhusika katika kashfa ya Richmond inayoendelea kulitia Taifa hasara ya mamilioni mpaka leo,

    ReplyDelete
  4. Mh Lowassa sina chuki nae lakini nadhani alama za nyakati amezipa kisogo aidha kwa bahati mbaya au makusudi, ningekuwa mimi ni mshauri wake ningemshauri aendelee na ustaafu wake. Tayari anatangaza nia ya kugombea urais huku akiwa ameshatengeneza ufa mkubwa katika kipindi cha ndani ya miaka kumi...apumzike!

    ReplyDelete
  5. Rais rais...

    Mdau wa nne, Nyufa zinatokana na tabia ya sisi watanzania kuwa wazembe wa kutopenda kufikiria, na kufanya kazi. Huyu jamaa yeye yuko tofauti ndiyo maana makundi yanatokea ya wale wapenda mabadiliko, na wale wanaopenda kuendelea kulala.

    Alama za nyakati hazijampa kisogo Lowassa, ndiyo wakati wake hasa. Tumeshaona makosa tuliyoyafanya miaka nane iliyopita, sasa ndiyo muda muafaka wa kuyarekebisha ili tusonge mbele.

    Huyu ndiye hasa tumtakaye, na anatufaa kwa sasa hapa Tanzania ilipofikia.....Tuwe wakweli hali ya utendaji ni mbaya sana serikalini na kwenye taasisi zake, bila mabadiliko tunaelekea shimoni.

    ReplyDelete
  6. Mh. Rais wangu Lowasa, niko nyumba yako kura yangu nakuongezea, wewe ni kudume bwana, nakumbuka nikiwa wizara fulani ulivyotengua mkataba wa maji bila ya woga, wewe ni kudume, songa mbele, usikate tamaa na maneno ya wanadamu, wao wameumbwa kusema, na hawataacha, najua ukiwa rais, pale katika kijiji changu cha manyamanyama bunda, utatuwekea umeme. usikate tamaa Mh. Rais. Bwana awajua walio wake, na urais bwana anajua utawasaidiaje watanzania. soma yeremia yeremia 1:19

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...