
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza katika tafrija aliyoiandaa kwa wananchi wake na wageni mbalimbali ya kuukaribisha mwaka mpya 2014,iliyofanyika jana nyumbani kwake Ngarashi Monduli.Pembeni yake ni mkewe mama Regina Lowassa.
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wageni waalikwa waliofika kwenye tafrija hiyo aliyoiandaa kwa wananchi wake na wageni mbalimbali ya kuukaribisha mwaka mpya 2014,iliyofanyika jana nyumbani kwake Ngarashi Monduli.
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) akizungumza na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mh. Goodluck Ole-Medeye wakati wa tafrija hiyo iliyofanyika jana nyumbani kwake Ngarashi Monduli.
Wageni waalikwa mbalimbali





barikiwa saana, ila naona ni watu wazito wazito tu, yatima na wasio na uwezo walikuwepo?
ReplyDeleteMh. Lowasa 'alistaafu' uwaziri lini na wapi?
ReplyDeleteHakuwahi kustaafu ila alilazimika kuacha kazi kwa kosa la kuhusika katika kashfa ya Richmond inayoendelea kulitia Taifa hasara ya mamilioni mpaka leo,
ReplyDeleteMh Lowassa sina chuki nae lakini nadhani alama za nyakati amezipa kisogo aidha kwa bahati mbaya au makusudi, ningekuwa mimi ni mshauri wake ningemshauri aendelee na ustaafu wake. Tayari anatangaza nia ya kugombea urais huku akiwa ameshatengeneza ufa mkubwa katika kipindi cha ndani ya miaka kumi...apumzike!
ReplyDeleteRais rais...
ReplyDeleteMdau wa nne, Nyufa zinatokana na tabia ya sisi watanzania kuwa wazembe wa kutopenda kufikiria, na kufanya kazi. Huyu jamaa yeye yuko tofauti ndiyo maana makundi yanatokea ya wale wapenda mabadiliko, na wale wanaopenda kuendelea kulala.
Alama za nyakati hazijampa kisogo Lowassa, ndiyo wakati wake hasa. Tumeshaona makosa tuliyoyafanya miaka nane iliyopita, sasa ndiyo muda muafaka wa kuyarekebisha ili tusonge mbele.
Huyu ndiye hasa tumtakaye, na anatufaa kwa sasa hapa Tanzania ilipofikia.....Tuwe wakweli hali ya utendaji ni mbaya sana serikalini na kwenye taasisi zake, bila mabadiliko tunaelekea shimoni.
Mh. Rais wangu Lowasa, niko nyumba yako kura yangu nakuongezea, wewe ni kudume bwana, nakumbuka nikiwa wizara fulani ulivyotengua mkataba wa maji bila ya woga, wewe ni kudume, songa mbele, usikate tamaa na maneno ya wanadamu, wao wameumbwa kusema, na hawataacha, najua ukiwa rais, pale katika kijiji changu cha manyamanyama bunda, utatuwekea umeme. usikate tamaa Mh. Rais. Bwana awajua walio wake, na urais bwana anajua utawasaidiaje watanzania. soma yeremia yeremia 1:19
ReplyDelete