Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akicheza draft na vijana wafanyabiashara wa soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya.
Nape yupo mjini Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM ambazo kitaifa zitasheherekewa mkoani hapo.
Katibu huyo wa NEC alikutana na vijana mbali mbali ambao walifurahi sana kumuona kiongozi wao akiwa pamoja nao kiasi soko zima lilipuka kwa nyimbo za hamasa za CCM zilizoimbwa na Kapteni John Komba,Nape pia alipata fursa ya kusalimiana na baadhi ya madereva wa Taxi wa kituo maarufu cha Mafiati.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na mpiga picha na blogger wa CCM Adam Mzee akila chakula cha mchana kwenye kibanda cha Mama Lishe anayefahamika kama Bi. Tandiwa Tewete kwenye soko la Sido Mwanjelwa mjini Mbeya.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikatiza katikati ya soko la Sido Mwanjelwa kwenda kwenye viwanja vya mpira vya soko hilo kushuhudia mechi ya mpira ya wafanyabiashara wa sokoni hapo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiangalia mechi ya mpira kati ya timu ya soka ya sokoni Sido wauza Mitumba na wafungua Mabelo kwenye uwanja wa mpira wa sokoni Sido.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa timu za mpira sokoni Sido Mwanjelwa mjini Mbeya mara baada ya mpira kumalizika.
The mdudu,mhh huyu ananikumbusha enzi za NYERERE(RIP) Nape amevunja rekodi anasitahiri sifa na pongezi kwa viongozi wetu wa sasa kamwe hawezi kula kwa mama nntilie,KUANZIA LEO nakuombeni wananchi wenzangu au watanzania wenzangu pasipo na itikadi za vyama mm nimeamua kumbadirisha jina TOKA NAPE KWENDA NYERERE WETU,angalizo kwa waosha vinywa mm hizo picha za Nyerere wetu zimenigusa vibaya sn mungu amlinde huyu Nyerere wetu coz mm inaniuma vibaya mno kuona viongozi waliochaguliwa na wananchi kisha viongozi hao hao wanawakimba watu waliowaweka madarakani ndio maana wengi wao wana vitambi hivyo vitambi ni mazambi yao wamebebeshwa na MUNGU mbona sisi wengine hatuna vitambi? JIBU LAKE coz sisi hatuzurumu vya watu.
ReplyDeleteMhe. Nape Nnauye,
ReplyDeleteUmetoa mfano mzuri sana ukiwa kama Kiongozi wa Ngazi za juu na Mwandamizi ndani ya CCM!
Ni vema Viongozi wa Chama na Serikali (WALIO ZOEA KULA NEW AFRICA HOTEL, KILIMANJARO HOTEL NA SERENA HOTEL) wakaanza kula Magengeni na kupunguza gharama za Kiserikali na Kichama ili tuweze kuendelea!!!
Kama Nape Nnauye uliwanyooshea kidole Mawaziri Miaigo na wakang'atuliwa, je kama wewe Kiongozi Mwandamizi ktk Chama chetu CCM unakula Gengeni kwa Mama Ntilie ni nani atakataa (ktk Ofisi ya Serikali ama Chama) na yeye kuwa asile kwa njia hiyo?
ReplyDeleteHakuna kama Nape Nnauye!
ReplyDeleteZaidi ya Lishe kwa Mama Ntilie Mbeya, nilifurahi ulipotumia Usafiri wa Baiskeli kule ktk Ziara ya Ukanda wa Ziwa Nyasa!!!
Tukipata nusu ya Viongozi ktk Chama na Serikali wenye mtindo wa maisha ya kawaida kama Mhe. Nape Nnauye nadhani tutaendelea sana!
ReplyDeleteSawa sawa Mhe. Nape Nnauye!
ReplyDeleteKama Uungwana ni vitendo, basi na pia Uongozi ni VITENDO!
Endapo wewe KATIBUY MKUU NEC UENEZI NAITIKADI Mhe. Nape Nnauye utakuwa kwa Mama Ntilie Gengeni ni nani tena katika Chama atakataa kula kwa Mama ntilie?
ReplyDeleteHuyo atakaye kataa moja kwa moja atakuwa sio mwenzetu!!!
Kuanzia leo ktk Ofisi za Chama na Serikali tutafuata Kiongozi wetu Nape anavyo bana matumizi.
ReplyDeleteAtakaye kataa tutamnyang'anya Kadi yetu!!!
Ebo, mbona kwenye Upinzani CUF na Chadema wananyang'anya Kadi Waanachama kwa makosa madogo madogo ama bila sababu za maana iwe sisi CCM kwa mtu kukataa kufuata msimamo na mwenendo wa Kiongozi wa juu kama kula Gengeni?
Kaka; Vijana na Watanzania wote tunatamani na tunapenda kula vizuri na kuishi vizuri. Najua Magengeni na Kwa Mama Lishe kunadharaulika. Nchi nyingine hata wafanyakazi wa IKULU utawakuta kwa mama Lisha na magengeni. Wewe ni shujaa wetu na ni Kiongozi wetu. Tunakuomba huku kwa mama Lishe kuwe bora ili maisha yetu yawe bora. Kuwe kusafi na kiafya ili tuendelee. Usibweteke na kula JUNK FOOD. Watu wanadhani kula chips zilizokaangwa kila siku ni afya. Hawajui hao. Kule kuku mayai mboga samaki na maziwa. Hivi hupatikana kwa mama Lishe kirahis na bei ni poa tu. Tunza afya yako Nape, jitunze na tunza heshima yako. Tuko nawe dama na TUNATAKA UTUONGOZE. Mifano ipo kuwa wewe ni Kiongozi bora.
ReplyDelete