Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda umeeleza kusikitishwa na taarifa za blog ya Rwanda “News of Rwanda” ambayo inaunga mkono serikali ya nchi hiyo iliyotolewa mwishoni mwa juma zikimtuhumu rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa kuunga mkono na kufanya mikutano na wanachama wa makundi ya waasi yanayopingana na serikali ya Rwanda.
Akizungumza na Sauti ya Amerika mkurugenzi wa mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania Salva Rweyemamu amesema wao wameshangazwa kwa sababu mwaka jana kulikuwa na matatizo na marais wa nchi hizo wameshazungumza vizuri wakakubaliana na kuonyesha kwamba sasa mambo yameisha na kwamba wanaendeleza urafiki wao, udugu wao na ujirani mwema wa miaka mingi kati yao na kuongeza kwamba hilo ni jambo la kusikitisha sana kwa upande wa Tanzania.
Ametoa wito kwa vyombo vya habari nchini humo visaidie kujenga uhusiano mwema na visiwe mwanzo wa choko choko ya kugombanisha watu akiuliza kuwa “Tanzania wakigombana na Rwanda magazeti yatauzwa?” au mkiwa kwenye hali ya vurugu kama ilivyo nchi zingine ambapo watu wanapigana kila siku kuna watu wananunua magazeti pale?
Kusikiliza mahojiano ya Salva Rweyemamu na VOA bofya hapo.
http://www.voaswahili.com/content/article/1841294.html
Vyombo vya habari visieneze habari zisizojenga uhusiano mzuri wa nchi na nchi.Habari kama hizi hazisaiidii uhusiano mwema wa majirani.
ReplyDeleteLakini kwa nini haya mambo yanatokea sasa...hili ni swali la msingi kujiuliza!
ReplyDeleteWamezowea kutumia vyomba vya habari kuleta vurugu. Si ndivyo vilitumika katika kuuana kwa mwaka 94?
ReplyDeleteSijui kwa nini baadhi ya wanahabari siku hizi wanapenda kuleta machafuko. Kun a kutoa habari na kuna kutoa habari zinazoamsha hisia za kuchoma mioya ya wasikilizaji na wasomaji.
Waswahili wanasema AMANI wanyarwanda wanasema AMAHORO. Tuishi kwa amani. Hakuna haja ya choko choko.
ReplyDeleteRwanda acheni kutapa tapa rekebisheni shinda zenu na malamiko ya Dunia dhidi yenu !
ReplyDelete-Ihakikishieni dunia ya kuwa Mauaji yaliyotoeka Afrika Kusini Januari mosi mwak huu 2014 kama Mamlaka za Kigali hazikuhusika.
-Kaeni na Waasi wenu ambao ni raia halali wa Rwanda mmalizane na muihsi pamoja kama ndugu, kama Marekani ina kaa na Taliban na Al-Qaeda iweje nyie RWANDA MSIKAE NA FDLR?
TANZANIA TUNATUMA MAJESHI NA KUSHIRIKI VITANI KULINDA AMANI TU,
UCHUMI WA VITA SIO MPANGO WETU WA KIMAISHA HAPA TANZANIA,
TANZANIA HATUTAKI VITA TUNATAKA MAENDELEO NA MAISHA BORA!