Mhe. Abdulkarim Shah, Mbunge wa Mafia, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Kamishna wa Tume ya Utumishi ya Bunge, anasikitika kutangaza kifo cha mama yake mzazi, Bi. Fatma Abdulkarim Mussa (pichani) kilichotokea Chennai, India tarehe 28 Januari, Mwili wa marehemu utawasili nchini tarehe 30 Januari, 2014 kwa ndege ya Shirika la Emirates, saa tisa alasiri na kuzikwa siku ya Ijumaa saa saba mchana katika makaburi ya Kisutu.

Msiba upo Magomeni, Mtaa wa Matombo, Mwembechai karibu na kwa Sheikh Yahya Hussein.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:

1. Mhe. Abdulkarim Shah - +918 015 026 119 (India)
2. Ndg Khalid Shah - 0715 567865
3. Ndg. Athumani Kwikima - 0759 683 421 - 0787 965 965/0759 305 739

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Inna Lillahi Wainna Ilayhi Rajiun. Poleni sana wafiwa, ndugu jamaa na marafiki wote wa marehem Bi Fatma Abdulkarim Mussa. Mwenyeez Mungu amraham mja wake, amughufirie kwa yote, amnusuru adhabuze na kesho 'Yaumul-Hisabu' awe ni miongoni mwa waja wake wema watakaoingia Jannatu Nnaeem yake - Ameen. Nasi sote tungalio njiani, Yarabi tunakuomba utujaaliye 'Khusni-l-khatima' Insha Allah, Ameen.

    ReplyDelete
  2. ameen Ya Rabbil alameen. Mungu akuandikie thawabu kwa dua zako ndungu. we really appreciate it
    JazakaAllah khairan

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...