Habari za kazi Ankal.

Katika kipindi cha wiki moja nimekuwa nikitazama tamthilia ya Kiswahili inayoitwa The team(wengi watakuwa wanaifahamu). Napenda kuwapongeza watayarishaji na waigizaji wa tamthilia hii kutokana na ufanisi waliouonyesha katika kuiandaa tamthilia.

 Kama Mtanzania nimevutiwa na kujivunia kwa mengi,mojawapo ikiwa ni matumizi fasaha ya lugha ya Kiswahili,kitu ambacho ni vigumu kukiona katika filamu zingine au katika maisha ya kila siku.

Hoja yangu ni juu ya majina yaliyotumiwa na waigizaji. Kulikuwa na Upendo,Waridi,Bahati,Sofia na mengine. Watanzania wengi na waafrika kwa ujumla tumekuwa na kasumba ya kuwapatia watoto wetu majina ya kigeni kama vile ya kizungu,kiarabu n.k, ambayo wakati mwingine hata maana zake hatuzijui. 

Hivi hakuna haja ya kuitana majina yetu wenyewe na kuthamini vilivyo vyetu kuliko kuiga kila kitu? Najua ni suala la kibinafsi lakini nimeona nitoe ya moyoni wadau.

Ni hayo tu Ankal.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hoja ya Msingi.Wenzetu waKurya bado wanayatumia sana.Kuna mdau humu alitoa comment miezi kadhaa imepita kwamba kwa Tanzania ukitumia jina la Ukoo unakosa ajira..!!.Kuna ukabila sana kwenye ajira za Tanzania(sehemu fulani fulani) ndiyo maana tumeachana na majina ya Kikabila

    ReplyDelete
  2. Asante sana mdau uliyeleta hii mada. Kusema ukweli nimekuwa nikikerwa sana na matumizi ya majina ya wenzetu (wakoloni). Kwa wakristo tunatumia ya wazungu, kwa waislamu naona zaidi wakitumia majina ya kiarabu. Huu ni utumwa wa fikra na muendelezo wa ukoloni. wenzetu wahindi walihakikisha wanatumia majina yao kwa asilimia kubwa hata kama wamingia hizi imani zetu.

    sula la mdau wa kwanza kuhusu ajira, ni kweli kuna ubaguzi lakini hili halitufanyi tusiwape watoto wetu majina ya asili.

    Mimi nilijaribu kuwapa watoto wangu majina ya asili ikawa mbinde huko kanisani na kwa ndugu (wa upande wangu na wa mke wangu). Wanataka majina ya kizungu. Kanisani wanataka majina ya watakatifu. Nilitii nikafanya walivyotaka laini ni utumwa wa fikra tulio nao waafrika. Tuache.

    ReplyDelete
  3. BAHATI, SOFIA, WARIDI ni ya kiarabu na kiyahudi.

    Mwandishi be informed kwanza.

    ReplyDelete
  4. ukiwa lofa utaiga jina la tajiri.
    ukiwa mjinga utaiga jina la merevu.
    ukiwa dhaifu utaiga jina la kawi.

    ReplyDelete
  5. Majina ya kikabila ni kweli yanahasara maana watoto watabuguliwa kikabila katika ajira huko mbele.

    Na pia majina ya kiarabu, kiyahudi na kizungu yana hasara ileile, ubaguzi.

    Huko mbele tutatafuta majina yasiyo ya dini, rangi, wala kabila.

    ReplyDelete
  6. Ndugu mleta hoja au mada ningekuomba angalau ukatutajia majina 10 unayoyaona wewe ni muafaka watu au watoto wetu tuwaite ili wachangiaji wajifarague zaidi katika kuyatafakari.

    ReplyDelete
  7. Mdau uliyesema majina ni ya kiyahudi na kiarabu inawezekana lakini ni ya Kiswahili pia kwa sababu maana zake japo ni za kutafasiri kutoka lugha za watu lakini tunazitumia katika Kiswahili. Mtoto akiitwa Faraja,Furaha au Upendo haiwezi kulinganishwa na majina kama yale ya kiustadh au kiupako zaidi. Watu tunafikia kuita watoto majina ya majini kama Maimuna...Uturuki maimun ni nyani kwa mfano. Wazungu tukiwaangalia japo wana dini kama hizi zetu lakini majina yao ni ya kiasili. ...angalia wacheza mpira ndiyo utapata picha (waitaliano,waspain,waingereza,wanorway,wasweden,warussia,wajerumani,wachina). Hata waislamu pia wana majina tofauti,mwarabu wa Yemen,Mpakistani, mwarabu wa Saudia, Waturuki, Wafarsi wa Irani,Waindonesia wote dini moja lakini majina tofauti. Kwa mdau uliyesema majina ya kikabila yanaleta ubaguzi katika ajira,inawezekana lakini hilo ni afadhali kuliko haya ya wakoloni ambayo ndiyo yameanza kusababisha machafuko na ni tiketi ya kufa au kuishi katika baadhi ya nchi kama Jamhuri ya Africa ya Kati na Nigeria. Nchi kama Afrika Kusini ambazo harufu ya Ubaguzi bado ipo ndiyo unaona wako makini. Ni sisi tu tumezidi ulimbukeni,kila kitu tawile baba tawile.

    ReplyDelete
  8. Nadhani hilo la majina ni kiashiria kimoja tu cha bidii ya kuikimbia asili yetu. Tumekumbwa na balaa la ajabu. Hata chakula cha asili tunakikimbia hata pale ambapo kuna sababau za kitaalam kabisha kwamba chakula cha asili kina ubora zaidi kilishe.Alafu tumefika hatua ya kutunga hata majina ya 'kizungu' amabayo kwa wazungu hayapo kabisa; kwa mfano: Godlove, Happiness, Godfear, Heavenlight... ni majina ya 'kizungu' amabyo wazungu wenyewe hawana. Ama kweli ni ulimbukeni kama wachangiaji waliotangulia walivyosema! Yani tunataka kuishi kmaisha ya kizungu amabayo hazungu wenyewe hawaishi... yani ni vitu tunavyofikirifikiri tu sisi wenyewekwamba ni uzungu. Sasa kama uzungu wetu unaishia kuwa uzungu wa kiafrika kwa nini tusikubali uafrika wetu tu na kuishi kwa namna ya ukweli, uthabiti na uhalisia?

    ReplyDelete
  9. Jina langu la pili ni la kikabila, nipo mamtoni kwenye fani ya tiba zaidi ya miaka ishirini sasa, sijawahi baguliwa kwa sababu ya ubin wangu, ubaguzi nilioupata ni kwa sababu mimi ni MPINGO, waingereza bwana kama zinachaji wanasahau kama wewe ni MPINGO, na in my case wamesahau sana, na ubaguzi unaupata toka kwa wazungu masikini wasio na elimu dunia.
    Kama nyumbani TZ inafika wakati Jina la ukoo noma, basi kwa kweli tunapoenda kubaya na Mungu arusaidie.

    ReplyDelete
  10. Anon wa 7,
    hivi unaamini kabisa shetani likimpanda mtu likasema jina lake itakuwa linasema kweli?

    kumbuka ni shetani hivyo haitakuwa ukweli?

    Mi siamini neno lolote lisemwalo na pepo.

    ReplyDelete
  11. Watanzania tuache ulimbukeni. Wazazi wetu walilazimishwa na wakoloni kuitwa majina ya kizungu eti yetu ya asili ni ya kishetani, amini usiamini mpaka kizazi chetu cha sasa kunawatu wanamini hivyo.

    nadhani serikali inabidi kuongeza bidii kwaelimisha wananchi somo la uraia ili watanzania waanze kujipenda na kujiamini.

    Hakuna majina ya dini ni upuuzi mtupu, na hizo excuses za uongo hazitakiwi tena.

    Mako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...