Balozi wa Tanzania BELUX na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika picha ya pamoja na mwakilishi wa kampuni ya ORIGO Bwana Lieven De Koker anayeshiriki Maonyesho ya Utalii ya Brussels. Bwana Lieven anakaa Arusha na kampuni yake inashiriki Maonyesho ya Utalii ya Brussels kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania na nchi nyingine za Afrika. Balozi Kamala ameishukuru Bwana Lieven kwa kazi anayofanya ya kutangaza utalii wa Tanzania.
Balozi wa Tanzania BELUX na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimsikiliza mwakilishi wa kampuni ya Utalii ya Reisspeciliast ya Ubelgiji akimweleza jinsi kampuni hiyo inavyopeleka watalii Tanzania mara mbili kwa mwaka na jitihada zinazofanywa na kampuni hiyo kuitangaza Tanzania Ubelgiji. Balozi Kamala ameishukuru kampuni hiyo na ameiomba iendelee kuitangaza Tanzania.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...