Bondia Habasi Hamisi wa Kigoma akikwepa konde la Mustafa Murinho  wakati wa mashindano ya Nelson Mandela Open Championship yaliyofanyika katika  viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam Morinho alishinda kwa point mpambano huo na kuingia fainal
Bondia Finias Genga kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Haruna Swanga wakati wa mashindano ya Nelson Mandela Openchampion ship yaliyofanyika katika viwanja vya  Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam Swanga alishinda kwa TKO ya raundi ya kwanza na kufanikiwa kuingia fainal ya mashindano hayo Picha Na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Haruna Swanga akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi wake
Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis akisaidia kufunga mlingoti wa taa katika mashindano hayo

Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT Mutta Rwakatare akimwelekeza ofisa habari wake Viduka  jinsi ratiba ya mahindano yanavyokwenda kushoto ni Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis
Diwani wa Kata ya Kawe Othumani Kipete Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis na  Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT Mutta Rwakatare wakifatilia kwa makini Mashindano hayo
Aisha Vonialis




Na Mwandishi Wetu Kawe

Mjumbe wa maendeleo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis amesema wanawake wanatakiwa wawe na msukumo mkubwa katika kuhakikisha wanajitokeza kwenye mchezo wa masumbwi.
akizungumza wakati wa mashindano ya kumuenzi Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini Nelson Mandela Open Boxing Championship yaliyofanyika katika viwanja vya  Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam. 

Mjumbe huyo alitoa wito kuwa wanawake wanaweza hivyo wajitokeze katika kucheza mchezo wa ngumi na kuangalia mchezo huo kama michezo mingine akitolea mfano unaona katika mashindano haya wanawake ndio walio ongoza kuja kwa wingi kwa kuwa wanapenda mchezo siku zote tulizo kuwepo hapa katika viwanja hivi wanawake wanakuja kushangilia sana tu.
aliongeza kwa kusema kuwa wanaomba mashilika,makampuni tasisi mbalimbali pamoja na watu binafsi kuja kusaidia mchezo wa masumbwi upate wadhamini wa kutosha kwani mashindano hayo yamekutanisha mikoa mbalimbali nchini kwa sasa hivyo wadau wote wanaombwa kujitokeza kudhamini mchezo huo.
katika mashindano hayo ya kuingia fainali bondia Mustafa Morinho alimsambalatisha Abbasi Hamisi uku Jonson Swanga akimpiga Disson Everest na Abuu Said akimdunda Frank Msindo na Haruna Swanga akimwazibu bila huluma bondia Finias Genga kwa TKO ya raundi ya kwanza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...