Hili ni gari...Chukulia hili gari kama usafiri wako katika kuendesha mahusiano yako na yule mweza umpendae. Humu ndani ya gari kuna familia yako yote na wewe ndiye dereva...Njia utakayochagua kulipitisha hili gari,ndio njia watakayopita familia yako
Gari hili lina matairi yanayokaribia kugusa ardhi...ni kama unaendesha Lamboghini vile...Very delicate! Endesha gari lako katika Njia iliyonyooka,utakutana na mabonde na milima,lakini usipokwepa hivi na kuingia njia za uchochoroni usikojua kuna matope kiasi gani,basi hii milima na mabonde itapita na njia itaendelea kunyooka.
Baki Njia Kuu, Michepuko Sio Dili
Epuka Ukimwi.
very creative and educational. Tushindwe wenyewe kufuata ushauri!
ReplyDeleteMdau Canada
Ushauri unatakiwa ulimbukeni usije ukapoteza wengi kisa kusherekea siku.
ReplyDeleteAma kweli wengi wanaendeshwa na Saikolojia ya ngono na ujinga!
ReplyDeleteLicha ya Maelekezo mazuri sana hapa na Mdau aliyetoa kigezo cha gari hilo, ile jana tu kwenye Valentine Day Matokeo kama haya hapo chini inawezekana sana kuwa yametokea:
1.Maambukizi mapya ya Ukimwi,
2.Usaliti kwa wenza wawili,
3.Hasara kubwa na ukwepaji wa majukumu kwenye Familia zetu kwa wenza hao wa gizani kuzitelekeza familia zao hata DONA kwa DAGAA wakakosa huku watu hao walio ibana kimahusiano wakiwa chemba wakila MAINI KWA MISHIKAKI YA MBUZI HUKU WAMEKUMBATIANA wakiwa Mafichoni!