Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea sehemu inayoingia maji ya chumvi katika eneo la Kilimani mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Zanzibar Sheha Mjaja Juma, akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, kuhusiana na kuingia maji ya chumvi katika eneo la Kilimani mjini Zanzibar.
Afisa Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja Dr. Makame Ali Ussi, akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, kuhusiana na kuingia maji ya chumvi katika eneo la Fungu refu, Mkokotoni.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akishuhudia hali ya uharibifu katika hoteli ya Zalu Nungwi, uliotokana na upepo mkali uliovuma katika Mkoa wa Kaskazini Unguja Jumapili usiku, na kusababisha majengo na maeneo kadhaa kuharibiwa vibaya.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea skuli ya Nungwi, kuangalia uharibifu uliotokana na upepo mkali uliovuma katika Mkoa wa Kaskazini Unguja Jumapili usiku, na kusababisha majengo na maeneo kadhaa kuharibiwa vibaya. (picha na Salmin Said, OMKR).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...